Na WAF - DODOMA

Waganga Wakuu wa Mikoa (RMOs) na Halmashauri wameulalamikia ubovu wa Mfuko wa Afya Ngazi ya Jamii (CHF) kutokana na kutokukidhi mahitaji ya wananchi kupata huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa RMOs Dkt. Best Magoma wakati akiwasilisa risala yake kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel (Mb) ambaye alikua mgeni rasmi katika mkutano wa RMOs uliofanyika leo jijini Dodoma.

Akijibu risala hiyo, Dkt. Mollel amesema ni kweli kumekua na malalamiko makubwa ya wananchi kutokupata huduma zinazokidhi viwango kupitia kadi za CHF.

"Kila ninapofanya ziara kwenye Mikoa na Wilaya napokea malalamiko juu ya madhaifu makubwa ya CHF na wananchi wanadhani ndio kadi za Bima ya Afya ya Taifa ya (NHIF)" amesema, Dkt. Mollel.

"Nakiri kuwa CHF ni tatizo kila mahali hata huko nilikofanya ziara wananchi wanalalamikia CHF na wengi wanasema BIMA YA AFYA ukiwambia leteni kadi zenu wanaleta za CHF ambazo siyo NHF" amesisitiza Dkt. Mollel

Dkt. Mollel amesema njia muafaka ya kuondokana na kero na malalamiko ya wananchi kwenye upatikanaji wa huduma ni kupitia muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote utaotoa nafasi kwa wananchi kupata huduma bora katika Hospitali zote nchini kuanzia Zahanati mpaka Hospitali ya Taifa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...