Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WIZARA ya Maliasili imetangaza kuwachukulia hatua Kali za kisheria baadhi ya maofisa wanaoshiriki katika biashara ya uvunaji haramu kwenye hifadhi za misitu katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro huku akieleza wamejipanga kuweka mikakati kuimarisha ulinzi.
Akizungumza leo Februari 20,2023 Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa wakati akikabidhi Pikipiki zaidi ya 40 kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) kwa ajili ya kutumika kuimarisha ulinzi, Mchengerwa amesema zipo taarifa kwamba kuna baadhi ya maofisa wamekuwa wakihusika kwenye uvunaji haramu,hivyo waache mara moja.
Waziri Mchengerwa alipokuwa akitoa kauli hiyo alikuwa ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mary Masanja pamoja na Katibu MKuu Dk.Hassan Abbas ambao walipokelewa na mwenyeji wao Kamishana wa Uhifadi TFS Profesa Dos Santos Silayo akiwa na maofisa wa idara mbalimbali za Wakala huo.
“Tunazo taarifa wako baadhi ya maofisa wetu wamekuwa wakishiriki kwenye biashara ambazo si nzuri ikiwamo uvunaji haramu, tunayo maelekezo ya moja kwa moja ya Makamu wa Rais, kuhusu tatizo kubwa la uvunaji katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Kwa hiyo nikuombe Mtendaji Mkuu TFS, hawa maofisa wanaohusika na mikoa hiyo katika maeneo ya hifadhi, wajitafakari."
Akifafanua zaidi Waziri Mchengerwa amesema kwamba kwa sasa wanakwenda kubadilisha mifumo yote ya utendaji wa kimazoea ili kuhakikisha kile kinachokusudiwa na viongozi wao kinatekelezwa.
Hivyo Kama wapo walikuwa na tabia ya kuzembea, watawapa muda wa kubadilika na iwapo watashindwa waseme ili nafasi walizopewa wapewe wengine wenye uwezo wa kuzifanya kwa uadilifu na uaminifu.
Amesisitiza kuwa Wizara hiyo inakwenda kubadili mfumo wa utendaji na kuomba wale wote wanaozembea kujitafakari kama wanaweza nafasi hizo au wapishe wapewe wengine huku akimuomba Profesa Silayo kuhakikisha maofisa wanaohusika katika mikoa hiyo ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam, katika maeneo ya hifadhi wajitafakari kwani anakwenda kubadilisha mifumo ya utendaji kazi.
Amefafanua kwamba kila Mtendaji atapimwaa kwa jinsi anavyoweza kutekeleza majukumu yake ya kazi na kila atakayeteuliwa kwenye nafasi yake hasa watendaji kwenye mikoa na wilaya, watapimw kwa utendaji wao.
Waziri Mchengerwa amesema katika hilo hakutakuwa na vitu vya kutokea kwa bahati, kila atakayeteuliwa atakuwa ni yule aliyeaminiwa anaweza kufanya kazi ya udhibiti hasa uvunaji haramu ambao umezuiliwa, mahusiano baina yetu na wananchi.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwataka watendaji wotekuacha kukaa ofisini na badala yake waende kusikiliza na kutatua changamoto zilizopo pamoja na kujenga uhusiano baina ya Wakala huo na wananchi. “Kama kuna sehemu tulikuwa tunatereza tukawa hatuko karibu na wananchi, sasa twendeni na tukawape elimu.
"Inawezekana wapo ambao walikuwa wanavuna pasipo taratibu huenda wengine taratibu hawazijui, tuwape elimu. Pia inawezekana tukabadilisha maisha ya wale wanoishi kwenye maeneo ya hifadhi.”
Pia Waziri Mchengerwa ameitaka TFS kuongeza udhibiti wa usimamizi ili iendelee kufanya vizuri zaidi kwenye uvunaji."Tunafahamu TFS inafanya vizuri kwenye uvunaji, lakini ninaamini mkiongeza nguvu zaidi katika udhibiti kwenye hifadhi zetu za misitu mtavuna zaidi .”
Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, ameeleza mipango mbalimbali waliyonayo katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao huku akiweka wazi pikipiki zaidi ya 40 walizokabidhi katika mikoa mbalimbali zitasaidia udhibiti na kuulinda hifadhi mbalimbali za misitu.
"TFS inapaswa kuwa na vifaa mbalimbali vya kusaidia utekelezaji wa shughuli zake kwa ufanisi zaidi ikiwamo vifaa vya zima moto, magari na tayari baadhi wanavyo ikiwamo boti kwa ajili ya shughuli zao.Tangu wameachana na utendaji kazi wa kiraia na kuwa katika utendaji wa kijeshi vifaa hivyo ni muhimu katika utekeleazji wa shughuli zetu."
Waziri Mchengerwa na Katibu Mkuu Dk.Abbas wameteuliwa kuongoza Wizara hiyo hivi karibuni baada ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri ambako kabla ya kupelekwa Wizara hiyo Mchengerwa na Dk.Abbas walikuwa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo .
Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa (katikati) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya Pikipiki zaidi 40 ambazo zinakwenda kutumika katika kusaidia katika shughuli za kulinda Uhifadhi kwa kutimiwa na watendaji wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Wengine katika picha hiyo ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja( wa pili kulia) wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Hassan Abbas na wa pili kushoto ni Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Profesa Dos Santos Silayo
Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya kuzungumza na maofisa na watumishi wa Wakala huo sambamba na kushuhudia tukio la kukabidhi Pikipiki zaidi ya 40 kwa Wakala huo .
Baadhi ya maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS)wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa alipokuwa akizungumza na watendaji na maofisa wa Wakala huo .
Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa akizungumza na maofisa na TFS baada ya kufika kwenye Ofisi za Wakala huo leo Februari 20,2021 kwa ajili ya kuzungumza nao na kueleza mipango yao katika kusimamia Wizara hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Hassan Abbas (kushoto) akielezea jambo baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa ( wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mary Masanja ( wa kwanza kulia)kuingia katika Ofisi ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Profesa Dos Santos Silayo ( wa pili kushoto).
Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufika Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya kuzungumza na maofisa na watumishi wa Wakala huo sambamba na kushuhudia tukio la kukabidhi Pikipiki zaidi ya 40 kwa Wakala huo .
Baadhi ya maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS)wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa alipokuwa akizungumza na watendaji na maofisa wa Wakala huo .
Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa akizungumza na maofisa na TFS baada ya kufika kwenye Ofisi za Wakala huo leo Februari 20,2021 kwa ajili ya kuzungumza nao na kueleza mipango yao katika kusimamia Wizara hiyo
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Hassan Abbas (kushoto) akielezea jambo baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mohemed Mchengerwa ( wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mary Masanja ( wa kwanza kulia)kuingia katika Ofisi ya Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Profesa Dos Santos Silayo ( wa pili kushoto).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...