Anaripoti Jane Edward, Arusha
Moja ya changamoto kubwa inayotajwa kuzikabili sekta binafsi na za umma nchini ni namna ya kukabiliana na Rushwa na ufisadi jambo linalopelekea kushindwa kufikia malengo na kusababisha hasara kwa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Taasisi ya wataalamu wa udhibiti wa Rushwa na ufisadi Ali Mabrouk mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku tano yaliyokutanisha wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na Maafisa utumishi ,wanasheria na wahasibu .
Amesema kuwa ili kutokomeza Rushwa na Ufisadi ni lazima viongozi kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa washirikiane kwa pamoja ili kuleta matokeo chanya.
"Nimefurahi kuona Rais wa Tanzania na Zanziba wakiwa msitari wa mbele katika kukemea vitendo vya Rushwa na ufisadi jambo lina dhihirisha kuwa sisi wataalamu tuna kazi nzito ya kufanya ili kukomesha vitendo hivyo"Alisema
Kwa upande wao washiriki wa Mafunzo yaliyotolewa na Taasisi ya ACFE-Tanzania,Haruna Mbululo amesema katika siku tano walizokuwepo wamejifunza aina mbalimbali za ufisadi katika maeneo ya kazi na namna ya kukabiliana nayo.
Ameongeza kuwa watanzania watarajie kuwa mambo ya ufisadi katika maeneo ya kazi yataisha kwa kuwa watakwenda kuyasimamia kikamilifu ili kulinda mapato ya taasisi zao na Taifa kwa ujumla.
Bi Mtumwa Idd Hamad ambaye ni mshiriki pia wa mafunzo hayo anasema ipo haja ya kujijenga katika maadili ili unapofanya kazi katika mataasisi hapa nchini uwe ni mwenye kufuata kanuni na taratibu hali itakayo punguza ufisadi katika nyanja zote.
Ali Mabrouk Rais wa Taasisi ya wataalamu wa udhibiti wa Rushwa na ufisadi (ACFE-TANZANIA) akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Rais ACFE -Tanzania akigawa vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya udhibiti rushwa na Ufisadi jijini Arusha.
Rais ACFE -Tanzania akigawa vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya udhibiti rushwa na Ufisadi jijini Arusha.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ACFE-Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...