Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema wiki ijayo kujibu mashataka kadhaa, ikiwa ni pamoja na kudaiwa kutoa malipo ya kumfumba mdomo nyota wa filamu za ngono kabla ya uchaguzi wa urais wa 2016.
Baraza kuu la mahakama la Marekani limepiga kura kumfungulia mashtaka Trump baada ya kuchunguza malipo ya dola 130,000 (kiasi cha shilingi milioni 304.2 kwa mwanadada Stormy Daniels katika jaribio la kununua kimya chake kuhusu madai ya kuwa naye uhusiano wa kimapenzi.
Trump, mwenye umri wa miaka 76, na mbaye amekanusha mshtaka dhidi yake, atakuwa rais wa kwanza au rais wa zamani wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya jinai.
Ofisi ya Wakili wa Wilaya ya Manhattan, Alvin Bragg, ambaye amekuwa akifuatilia uchunguzi huo, ilithibitisha kwamba iliwasiliana na wakili wa Trump ili "kuratibu kujisalimisha kwake" kwa mashtaka ambayo hayakutajwa.
Taarifa kutoka Marekani zinasema kwamba Rais huyo wa zamani, anayeishi Florida, anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne, ambapo kuna uwezekano wa kurekodiwa alama za vidole na kupigwa picha kama washtakiwa wote katika kesi za uhalifu.
Trump amemsuta wakili wa wilaya ya Manhattan na kumwita mwendesha mashtaka huyo kama "fedheha", na kumshutumu kwa "kufanya kazi chafu ya Joe Biden".
Mashtaka katika hati ya mashitaka yatasomwa kwake kwenye usikilizwaji wa kesi hiyo, ambayo itadumu kama dakika 10-15, huku Idara ya Usalama wa Taifa maarufu kama ‘Secret Service’ yenye jukumu la kuwalinda marais wanaohudumu na marais wa zamani wa Marekani ndiyo itakuwa na jukumu la kulinda usalama wakati wa kesi hiyo ya kihistoria.
Trump, ambaye anajulikana kwa kusema ovyo, amemsuta wakili wa wilaya ya Manhattan, akimwita mwendesha mashtaka huyo kama "fedheha", na kumshutumu kwa "kufanya kazi chafu ya Joe Biden".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...