Leo Machi 30, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) ameongoza Maafisa Habari katika mchezo wa mpira wa miguu kati ya Maafisa Habari Mashabilki wa Simba na Maafisa Habari Mashabiki wa Yanga uliofanyika katika kiwanja cha Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo umeisha kwa ushindi wa magoli Matatu (3) kwa upande wa Maafisa Habari wa Yanga uku kinara wa Magoli akiwa ni Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Gerson Msigwa kwa kufunga magoli mawili kati ya matatu yaliyofungwa na timu hiyo huku Maafisa Habari Mashabiki wa Club ya Simba wakitoka na sifuri

Mchezo huo umechezwa baada ya kufungwa kwa Kikao Kazi cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikali, 2023 kilichofunguliwa Siku ya Jumatatu 27 Machi,  2023 na kufungwa leo Machi 30, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC)







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...