Njombe
Mahakama ya Hakimu mkazi Njombe,imefunga ushahidi wa kesi No 2 ya mwaka 2022 ya madai ya fidia ya Milioni 100 dhidi ya kanisa KKKT Dayosisi ya kusini iliyofunguliwa na msimamizi wa mirathi wa marehemu Kaselida Mlowe baada ya kifo kilichotokana na ajali,Hukumu kutolewa April 18,2023.
Kesi hiyo ya madai imefikia hatua ya kutolewa hukumu baada ya kusikiliza mashahidi ambapo awali Mahakama ilianza kusikiliza shahidi mmoja Bi,Siglada Mligo katika upande wa mdai huku upande wa utetezi ambaye ni Kanisa la KKKT Mahakama ikiwasikiliza mashahidi wawili ambao ni Rajab Kitwana (35) aliyekuwa dereva wa gari ya Kanisa pamoja na Petro Kilima (41) ambapo pande zote hazikukusudia kuongeza ushahidi na kisha Mahakama kufunga utetezi huo.
Kesi ilifunguliwa baada ya msimamizi wa mirathi kushinda kesi ya makosa ya usalama barabarani kesi No 6,2021 kutokana na ajali iliyotokea eneo la Kibena mlima wa Ichunilo mjini Njombe September 25,2020 ikihusisha gari aina ya Hiace yenye Namba za usajili T298 DNE na gari yenye Namba T210-AHU Mercedes Benz Track Mali ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini na kupelekea kifo cha Kaselida Mlowe.
Kesi hiyo imeendeshwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Njombe Lihad Chamshama huku upande wa madai ikiwakilishwa na mawakili watatu akiwemo Emmanuel Chengula,Frank Ngafumika na Gervas Semgabo huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Marco Kisakali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...