Mwalami na wenzake waomba upelelezi dhidi ya kesi yao ya dawa za kulevya ukamilike haraka

UPANDE wa utetezi katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya inayomkabili aliyekuwa kocha wa makipa wa klabu ya Simba Mwalami Sultan na wenzake watano, wameiomba Jamuhuri kuharakisha upelelezi dhidi ya kesi yao hiyo ili wateja wake wajue hatma yao.

Wakili wa utetezi Daudi Mzeli amedi hayo leo Machi 30,2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu.

Mzeli amedai kuwa wateja wake wapo ndani kwa zaidi ya miezi mitano na kwa muda mrefu shauri hili kila likija upande wa jamhuri wanakuja na majibu hayo hayo hivyo aliomba wajitahidi kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.

Mapema wakili wa serikali Caroline Matemu alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado unaendelea hivyo ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo nyingine kwaajili ya kutajwa.

Mbali na Mwalami washitakiwa wengine mmiliki wa Kituo cha michezo cha Cambiasso, Kambi Zuberi, Maulid Zungu, Said mwantiko, John Andrew na Sarah Joseph wote wakazi wa Dar es salaam.

katika kesi hiyo washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Katika shitaka la kwanza inadaiwa kuwa Oktoba 27, mwaka huu maeneo ya Kivule wilayani Ila, Dar es Salaam walikutwa na dawa za kulevya aona ya heroin zenu uzito wa Kilogramu 27.10.

Katika shitaka la pili, washitakiwa hao wanadaiwa Novemba 4, mwaka huu maeneo ya Kamegele Mkuranga mkoani Pwani, walikutwa na dawa hizo zenye uzito wa Kilogramu 7.79

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 13, Mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...