NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa benki ya NBC, James Meitaron (wa pili kulia) wakimkabidhi kombe mshindi wa kwanza wa mashindano ya NBC Lugalo Open 2023 Ally Mcharo kutoka klabu ya TPC, Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jeshi vya Gofu Lugalo, Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Generali mstaafu Michael Luwongo na Rais wa TLGU, Queen Siraki




NBC imekuwa ikifadhili michezo mbali mbali kiwa ni pamoja na ligi ya Kuu ya Tanzania bara, Dodoma Marathon n.k. Ligi yetu kwa sasa ni moja ya ligi zinazotajwa kuwa ni ligi bora barani Afrika na hii imewezekana kutokana na mchango wabenki ya NBC,” alisema Mhe. Mwinjuma. Aliongeza: “Ni rai yangu kwa NBC kuendeleza kuweka mkono kwenye michezo yetu na kwenye sehemu nyingine za kijamii hapa nchini.
Makampuni na taasisi nyingine pia ziige wanachokifanya benki ya NBC ili tuweze kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi,” Naibu Waziri aliipongeza NBC kufadhili michezo mbali mbali “Sikutegemea kuwakuta kwenye gofu, nimefurahishwa na jitihada zenu kwa kuwa mstari wa mbele katika kukuza na kuimarisha michezo Tanzania. Hongereni sana NBC nyinyi ni mfano wa kuigwa,” aliongeza Mhe. Mwinjuma.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...