Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema kuwa bajeti zinazotolewa lazima kuzingatia mrengo wa kijinsia kwa kuwa na bajeti inayoonekana kusaidia kufanya ufatiliaji

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi wakati akifungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa Wakuu wa Idara ya Mipango, Maafisa Utawi wa Jamii, Wakuu wa Idara ya maendeleo , maafisa Dawati la Jinsia, Maafisa maendeleo ya jamii Uwezeshaji kiuchumi, Maafisa Maendeleo wa Kata na Madiwani yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa Upangaji wa bajeti, mipango na Sera zinazozingatia Jinsia miongoni mwa watoa maamuzi pamoja na kutambua mapengo yaliyopo kwenye eneo la ushawishi na kujenga uwezo wa stadi za utetezi kwa siku za usoni.

Lilian amesema kuwa makundi yanayoshiriki wanaamini wako sehemu ya kufanya maamuzi ya kuhakikisha bajeti inayotoka katika maeneo yao inzingatia jinsia kutokana na uchambuzi mbalimbali unaofanywa katika Manispaa ,Miji pamoja na Halmashauri.

Amesema katika Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025(TDV 2025) imetambua kuwa mojawapo ya vichocheo vya ukuaji wa uchumi ni pamoja na jamii yenye muono wa kimaendeleo ambapo pamoja na mambo megine unakuwa na tamaduni wezeshi hususani kwa wanawake na makundi mengine.

Pia amesema haki za binadamu na za wanawake zinajadilwa kwa sababu wanawake hawajawa kwenye nafasi na fursa sawa kama ya wanaume kwani bado wananyanyaswa na kukandamizwa na kuonewa na mifumo ya maisha iliyopo hivyo wamekutana ili kubainisha changamoto zilizopo wakati wa upangaji wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia.

“Mnakutana leo ili kupeana mrejesho kuhusu utekelezaji wa masuala muhimu tuliyokubaliana katika mafunzo yaliyofanyika Desemba ya mwaka 2022 kuhusuiana na Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa Harmashauri ili kubainisha changamoto na mafanikio tuliyokutana nayo wakati wa utekelezaji wa kile tulichojifunza ikiwemo na kutengeneza mpango wa utekelezaji masuala muhimu tuliyokubaliana” alimesema Liundi

Warsha hii imejumuhisha washiriki kutoka Dar es Salaam na Shinyanga kwenye Halmashari na Manispaa za jiji kama vile Halmashauri ya Kishapu, Jiji la Ilala, Manspaa ya Ubungo pamoja na Kinondoni.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Mipango, Maafisa Utawi wa Jamii, Wakuu wa Idara ya maendeleo, maafisa Dawati la Jinsia, Maafisa maendeleo ya jamii Uwezeshaji kiuchumi, Maafisa Maendeleo wa Kata na Madiwani mara baada ya kufungua mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza wakati kufungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa Wakuu wa Idara ya Mipango, Maafisa Utawi wa Jamii, Wakuu wa Idara ya maendeleo, maafisa Dawati la Jinsia, Maafisa maendeleo ya jamii Uwezeshaji kiuchumi, Maafisa Maendeleo wa Kata na Madiwani yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TNGP) Lilian Liundi alipokuwa anafungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa Wakuu wa Idara ya Mipango, Maafisa Utawi wa Jamii, Wakuu wa Idara ya maendeleo, maafisa Dawati la Jinsia, Maafisa maendeleo ya jamii Uwezeshaji kiuchumi, Maafisa Maendeleo wa Kata na Madiwani yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...