Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeandaa mafunzo ya bajeti yenye mrengo wa Kijinsia kwa Asasi zisizo za Kiserikali yenye lengo kubwa la kuwajengea uelewa washiriki kuhusu dhana mbalimbali za usawa wa kijinsia yaliyoanza leo tarehe 28 hadi Machi 31 mwaka 2023.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya dhana na umuhimu wa Bajeti yenye mrengo wa kijinsia pamoja na kutambua mbinu mbalimbali za uchambuzi wa bajeti ya Kijinsia pamoja na kushirikishana uzoefu juu ya changamoto za uandaaji wa Bajeti zenye mrengo wa kijinsia.

Liundi amesema mafunzo hayo ni kwaajili ya kuimarisha ujuzi wa azaki katika kushawishi sera, mipango na bajeti zinazozingatia usawa wa kijinsia ikiwa ni pamoja na mbinu za kujengea uwezo jamii wa kushawishi Sera, mipango na bajeti yenye mrengo wa kijinsia pamoja na kushawishi na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika kuingia kwenye uongozi na ngazi za maamuzi.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza wakati kufungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa wadau mbalimbali wa Asasi zisizo za Kiserikali  yaliyoanza leo tarehe 28 hadi Machi 31 mwaka 2023 yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi alipokuwa anafungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa wadau mbalimbali wa Asasi zisizo za Kiserikali  yaliyoanza leo tarehe 28 hadi Machi 31 mwaka 2023
yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.
 Mwezeshaji wa masuala ya Jinsia na uwezeshaji- GAI Idd Mziray akiwasikisha mada kuhusu masuala ya kijinsia wakati Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa wadau mbalimbali wa Asasi zisizo za Kiserikali  yaliyoanza leo tarehe 28 hadi Machi 31 mwaka 2023 na kufanyika katika ukumbi wa TGNP leo jijini Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...