Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshukuru ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi anayoongoza ya Tanzania na Marekani, ushirikiano unaoleta manufaa makubwa katika Sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Afya.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wa Mataifa mbalimbali, Ikulu nchini Tanzania mbele ya Makamu wa Rais wa Marekani, Mhe. Kamala Harris, Dkt. Samia amesema katika Sekta ya Afya, maambukizi hatari ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Kifua Kifuu (TB) kwa sasa havitishii maisha ya wananchi wa Tanzania.
“Maambukizi ya Ukimwi yameshuka, kutoka asilimia 7.2% mwaka 2012 hadi kufika asilimia 4.7% mwaka 2016 hadi 2017, maambukizi haya yamepungua zaidi mwaka 2021,” amesema Dkt. Samia.
“Maambukizi ya Kifua Kikuu (TB) yameshuka kutoka watu 306 kati ya kila watu 100,000 hadi kufikia watu 208 kwa kila watu 100,000,” ameeleza Dkt. Samia
Aidha, Dkt. Samia ameeleza kuwa kwa sasa Wanawake wajawazito wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania wana uhakika wa kujifungua Watoto wasiokuwa na maambukizi ya Virusi hivyo, yote ikiwa ni jitihada na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Marekani.
Hata hivyo, Dkt. Samia amemueleza Mhe. Kamala kuwa vifo vya vinavyotokana na Malaria vimepungua kutoka idadi ya Milioni 7.7 tangu mwaka 2015 hadi kufika Milioni 3.5, ikiwa ni pungufu ya zaidi ya nusu ya vifo hivyo vinavyotokana na Malaria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...