Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Balozi Ali Idi Siwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa
Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF. Balozi Siwa alisisitiza uboreshaji wa
huduma bora kwa wanachama, kuendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi,
kuongeza kasi ya ukuaji wa Mfuko kwa kuifikia sekta binafsi na sekta
isiyo rasmi na kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utendaji kazi. Lengo
la mkutano huo ni kupitia Mpango wa mwaka ujao wa fedha na bajeti kwa
mwaka 2023/2024, ikiwa ni ushirikishwaji wa wafanyakazi katika maamuzi
ya kiutendaji. Ufunguzi wa mkutano huo umefanyika tarehe 18 Aprili 2023
katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba,
akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 50 wa Baraza Kuu
la Wafanyakazi uliofanyika jijini Arusha. Mkutano huo ulifunguliwa na
Balozi mstaafu Ali Idi Siwa ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
NSSF.Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala wa NSSF, Ekwabi Mujungu, alipata fursa ya kutoa salamu katika mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la NSSF. Mujungu amesisitiza kuendelea kusimamia maslahi ya wafanyakazi na pia alitoa wito kwa wafanyakazi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma.
Katibu Msaidizi wa Sekta ya Taasisi za Fedha TUICO, Victor Leonard Kom akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wajumbe wa Mkutano w Baraza kuu la Wafanyakazi wa NSSF. Mabaraza ya wafanyakazi yapo kisheria kwa madhumuni ya kutoa ushauri na kusimamia haki na ustawi sehemu za kazi
Wajumbe wa mkutano wa 50 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakifuatilia kwa makini mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha.








.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...