Benki ya Taifa ya Biashara (NBC Bank) ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi
Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana ilinogesha
shangwe za mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga kwa kuwapeleka
uwanjani wateja wake pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo ili kushuhudia
mtanange huo ulioisha kwa timu ya Simba SC kuibuka na ushindi wa 2-0.
Zaidi,
benki hiyo pia iliandaa ‘Screen’ kubwa kwenye baadhi ya maeneo ya
jijini Dar es Salaam ikiwemo Bar ya Warehouse Arena (zamani Nextdoor
Arena) iliyopo Masaki jijini humo ili kutoa fursa kwa wapenzi wa mchezo
huo ambao hawakuweza kufika uwanjani ili waweze kufurahia mechi hiyo.
Akizungumzia
hatua hiyo Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki
Masuke alisema huo ni mwendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kutumia
mechi hizo maarufu kama ‘Derby ya Kariakoo’ kuandaa matukio yanayolenga
kuwakutanisha na wateja wao wakubwa na wadogo ili kufurahia ladha ya
ligi hiyo inayoendelea kujiongezea umaarufu barani Afrika kufuatia
udhamini mnono uliofanywa na benki hiyo.
“Umekuwa ni utaratibu
wetu sasa kufurahia na wateja wetu kwa namna mbalimbali inapofika siku
kama ya leo ambapo miamba miwili ya Soka letu inapokutana uwanjani. Kwa
kutambua ile pressure wanayokuwa nayo wateja wetu kwenye mechi hizi
tumekuwa tukiwaandalia matukio kadhaa ili tu tuwe nao karibu siku hiyo
kubwa.’’ alisema.
Aidha jana kama ilivyokuwa kwenye derby
iliyopita, ilishuhudiwa wateja hao wakipata chakula cha mchana Hoteli ya
Hyatt the Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam sambamba na viongozi
wa benki hiyo tukio lilitofuatiwa na msafara maalum wa ‘marafiki’ hao
kuelekea Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mtanange huo kwa udhamini
wa benki hiyo kabla ya kurejeshwa wakiwa salama baada ya kuisha kwa
mechi hiyo.
“Kwa wale ambao wanakosa nafasi hii ya kufika
uwanjani pia tunawaandalia mazingira mazuri kwa kuwawekea screen kubwa
kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo bar maarufu zilizopo karibu na maeneo
yao,’’ alisema Bw Masuke
Mbali na kutoa fursa kwa wapenzi wa
soka kufuatilia mechi hiyo kupitia screen kubwa pia wateja hao walipata
fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia
maofisa wa benki hiyo waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo
kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa
maeneo hayo pamoja na viunga vya vya uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (Kulia) akizungumza na baadhi wa wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha mchana muda mfupi kabla ya wateja hao kuelekea Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi ya Derby katika Simba na Yanga iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikiwa muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kutoa fursa kwa wateja wake ambao ni wapenzi wa mchezo huo waweze kufurahia mechi za ligi Kuu ya Tanzania Bara inayodhaminiwa na benki hiyo.
Kama ilivyokuwa kwenye derby iliyopita, ilishuhudiwa wateja hao wakipata chakula cha mchana Hoteli ya Hoteli ya Hyatt the Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam sambamba na viongozi wa benki hiyo tukio lilitofuatiwa na msafara maalum wa ‘marafiki’ hao kuelekea Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mtanange huo kwa udhamini wa benki hiyo kabla ya kurejeshwa wakiwa salama baada ya kuisha kwa mechi hiyo
Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele akiwaaga mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kukamilika kwa mechi hiyo.
Beki wa timu ya Simba Henock Inonga akijipongeza kwa ushindi wa goli 2 -0 ambao timu yake iliupata dhidi ya wapinzani wao timu ya Yanga.
Zaidi, benki hiyo pia iliandaa ‘Screen’ kubwa kwenye baadhi ya maeneo ya jijini Dar es Salaam ikiwemo Bar ya Warehouse Arena (zamani Nextdoor Arena) iliyopo Masaki jijini humo ili kutoa fursa kwa wapenzi wa mchezo huo ambao hawakuweza kufika uwanjani ili waweze kufurahia mechi hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NBC wakifurahi pamoja na mashabiki wakati wa mechi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...