Benki ya Stanbic na UNDP Tanzania wametangaza ushirikiano wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa mtaji na huduma za maendeleo ya biashara kwa kampuni changa na biashara ndogo na kati za Kitanzania.
Ushirikiano huu, chini ya mipango yao ya
Stanbic Biashara Incubator na Funguo Innovation Programme, unalenga
kuboresha ubora wa huduma za maendeleo ya biashara zinazotolewa na watoa
huduma tofauti na waendeshaji wa uvumbuzi kwa kampuni na biashara
changa zinazoongozwa na vijana na wanawake. Vilevile, unalenga kukuza na
kusaidia mazingira yatakayoruhusu kampuni hizi kustawi.
Kadhalika,
ushirikiano huu unalenga kutoa mafunzo ya kiufundi, na kujenga uhusiano
na wawekezaji na wafadhili na kuongeza fursa kwa kampuni changa na
biashara ndogo na kati ili kuongeza vyanzo mbalimbali vya mtaji.
Utiaji
Saini wa hati ya makubaliano, yaani Memorandum of Understanding
ulifanyika kwenye hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa
ubunifu na ujasiriamali, kutoka sekta ya umma, sekta binafsi, wadau wa
maendeleo, waanzilishi wa kampuni za kibunifu pamoja na wandishi wa
habari.
Kusainiwa kwa hati hii kuliashiria kuanza rasmi kwa
ushirikiano huo na kuanza kwa shughuli ya kwanza ya pamoja, ambayo
ilihusisha mafunzo ya siku mbili juu ya mbinu na maarifa ya kutafuta
mitaji ya uwekezaji kwa kampuni changa na biashara ndogo na za kati.
Ushirikiano
huu unaendana na Lengo la 17 la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja
wa Mataifa, ambalo linasisitiza ushirikiano kwa maendeleo endelevu. UNDP
Tanzania na Benki ya Stanbic Tanzania wanatambua kuwa ushirikiano ni
muhimu katika kuendeleza mfumo wa uvumbuzi na ujasiriamali wa
Kitanzania, na wamejitolea kufanya kazi pamoja kukuza maendeleo endelevu
kupitia ushirikiano.
Akizungumza juu ya ushirikiano huu, Bi.
Christine Musisi, Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, alisema,
"Tunafurahi kushirikiana na Benki ya Stanbic Tanzania kukuza ubunifu na
ujasiriamali nchini Tanzania.
Tunaamini ushirikiano huu
utatusaidia kuongeza ufikiaji wa mtaji na huduma za maendeleo ya
biashara kwa kampuni changa na biashara ndogo na kati za Kitanzania,
hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wa Kitanzania, na hatimae
kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi."
Vivyo hivyo, Bw. Kevin
Wingfield, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, alisema,
"Tunafurahi kushirikiana na UNDP Tanzania kwenye mpango huu. Kama benki,
tumejitolea kuunga mkono wajasiriamali na biashara ndogo ndogo, na
tunaamini kuwa ushirikiano huu utasaidia sana kuongeza ufikiaji wa mtaji
na huduma za maendeleo ya biashara kwa kampuni changa na biashara ndogo
ndogo na kati za Kitanzania.”
Mwakilishi
Mkazi wa UNDP Bi, Christine Musisi (Wapili kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa benk ya Stanbic Tanzania Bw Kevin Wingfield (Wapili Kulia)
wakisaini mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika kuimarisha
upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwawezesha wafanyabiashara
waanzishaji,wakati na wadogo kukuza biashara zao kupitia programu ya
UNDP Funguo na Stanbic Biashara Incubator. Pichani kulia ni Mkuu wa
kitengo cha StanbicBiashara Incubator Kai Mollel na kushoto ni Meneja
Mradi wa programu ya Funguo Joseph Maniraliza
Mwakilishi
Mkazi wa UNDP Bi, Christine Musisi (Wapili kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa benk ya Stanbic Tanzania Bw Kevin Wingfield (Wapili Kulia)
wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya kushirikiana katika kuimarisha
upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwawezesha wafanyabiashara
waanzishaji,wakati na wadogo kukuza biashara zao kupitia programu ya
UNDP Funguo na Stanbic Biashara Incubator. Pichani kulia ni Mkuu wa
kitengo cha Stanbic Biashara Incubator Kai Mollel na kushoto ni Meneja
Mradi wa programu ya Funguo Joseph Maniraliza
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...