Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin akikabidhi kiasi Cha Tsh Milioni 2
Kwa uongozi wa Timu ya Mkwawa Queens inayocheza Ligi kuu ya Soka la
wanawake Tanzania inayotarajia kusafiri jumapili kwenda Dar,Kucheza na
Simba Queens kiasi Cha TshMilioni 3.4 zinahitajika ambazo zilikuwa
zikihitajika Kwa ajili ya safari hiyo .
Akikabidhi
msaada huo Leo Kwa uongozi wa timu hiyo ,Yassin alisema chama Cha
Mapinduzi kinatambua mchango mkubwa wa Timu ya Mkwawa Queens na Timu
nyingine Katika michezo na kuwa kutokana na changamoto ya timu hiyo .
Hivyo
alisema Katika kuunga mkono jitihada za Timu hiyo na jitihada za Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan Katika kuendelea michezo nchini wao kama CCM
mkoa wa Iringa wataendelea kuuunga mkono jitihada hizo ikiwa ni pamoja
na kusaidia sekta ya michezo ndani ya mkoa wa Iringa.
Alisema
jitihada za Mkwawa Queens wanaziona na kuwa ili Timu hiyo kutimiza vema
majukumu yake ni vema wadau kuendelea kuunga mkono Timu zote ndani ya
mkoa .
"Niwapongeze
Sana Uongozi wa Mkwawa Queens Kwa kuendelea kuwakilisha mkoa Katika
soka la wanawake na sisi kama chama tupo pamoja "
Aidha
Yassin alimpongeza mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego pamoja na
Viongozi wengine wa mkoa huo Kwa kuendelea kusaidia Timu .
Afisa habari wa Mkwawa Queens Francis Godwin alipongeza mchango huo wa chama na kuwa huo ni mchango mkubwa Kwa Timu kupokea .
Alisema
Kwa Sasa Timu hiyo inasafari ya kwenda Dar es salaam kucheza na Simba
Queens siku ya Jumanne na kuwa timu itaondoka Iringa Jumapili safari
ambayo itaigharimu Timu Tsh Milioni 3.4 baada ya hapo inajiandaa Kwa
mchezo wake Dodoma na Mkoani Lindi ambako ili kufanikisha Mzunguko
uliobaki zaidi ya Tsh Milioni 10 zinahitajika .
Hivyo
aliwaomba wadau kuendelea kuisaidia Timu hiyo na kumpongeza jitihada za
mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego na uongozi wa CCM mkoa chini ya
Mwenyekiti Daud Yassin na wote ambao wameendelea kuichangia Timu hiyo .
Godwin
pia alimpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati Kwa
mchango wake wa Tsh 200,000 na wote wanaondelea kujitolea Kwa ajili ya
Timu akiwemo katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazin Jackson Mnyawami
kuchangia Timu namba hii 0715621222 jina la mpokeaji Maryam Swaleh
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...