CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Amana chini ya Mwenyekiti wake Balozi Kindamba wamefanya ziara katika Hospitali ya Amana na kutoa vifaa tiba kwa wagonjwa ikiwemo 'Urine Container,' Taulo za mikojo na sanduku ya bomba za dripu.
Ziara hiyo iliambatana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata Ndg. Sabry Shariff na Diwani wa Viti Maalum Mhe. Aisha Isaa na Mhe. Zainabu Orty.
Aidha ziara hiyo ililenga kuwafariji wagonjwa ambapo wamewasikiliza changamoto zao na kuahidi kuzipeleka sehemu husika na kuweza kushughulikiwa.
👇👇👇👇👇
PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO HILO
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Amana ndugu Balozi Kindamba akizungumza jambo na mwenyeji wake Mganga mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa -Amana ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji wa Mifupa,Bryceson Loti Kiwelu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...