Dirisha la maombi kwa watanzania wanaotaka kushiriki mashindano ya wazi ya ubunifu kwa mwaka 2023 ya Visa Everywhere Initiative (VEI) limefunguliwa rasmi ambapo wavumbuzi wachanga na watoa huduma za fedha wachanga kwa njia ya mtandao (fintechs) watashindanisha uvumbuzi wao katika kutatua changamoto za kufanya malipo na biashara.

Mbali na tuzo za fedha, washindi wa VEI Tanzania watapata fursa kukutana na washiriki wa mtandao mkubwa wa Visa katika sekta za benki, biashara na sekta nyingine za kiserikali, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkazi wa Visa, Salma Ingabire. 

Pia, washindi watafaidika kwa kutambuliwia na majina makubwa ya biashara yanayoaminiwa na kuthaminiwa zaidi ulimwenguni. 

Fainali za Ulaya ya Kati na Mashariki, Mashariki ya Kati na Afrika (CEMEA) zitaoneshwa mubashara July 27, 2023 kupitia TechCrunch, gazeti maarufu la mtandaoni la Marekani lililojikita katika kuripoti masuala ya teknolojia na wavumbuzi wachanga. Kampuni itakayoshinda kutoka CEMEA itapata fursha ya kushiriki katika fainali za dunia zitakazofanyika Septemba 19, 2023 katika kongamano la biashara lijulikanalo kama TechCrunch Disrupt, huko San Francisco, Marekani.

Kwa mara ya kwanza mwaka huu, VEI CEMEA itatoa tuzo ya Risk and Security domain-Fintechs Innovating in Risk Excellence, au tuzo ya ‘FIRE’. Kupitia mashindano haya maalumu, Visa kwa kushirikiana na Emirates NBD wanakusanya kazi za wadau wa fintech duniani kwenye maeneo ya utambuzi na uthibiti wa udanganyifu, usalama mtandaoni na hatari ya kupoteza fedha kutokana na wakopaji kushindwa kulipa mikopo. 

Kufuatia mapitio ya pamoja kati ya wawakilishi wa Visa na Eemirates NBD, mshindi wa Fintech atapokea tuzo ya $25,000 na kupata fursa ya kufanya kazi na Emirates NBD.

“Visa Everywhere Initiative ni jukwaa linalowawezesha watoa huduma za fedha wachanga na wajasiriamali kuonesha ufumbuzi/uvumbuzi wenye msaada mkubwa katika kufanya malipo na biashara,” alisema Salma Ingabire.

“Kupitia utatuzi wao kiteknolojia na kibunifu, fintechs wana nafasi ya kuleta manufaa makubwa kwa jamii katika masoko wanayotumia, hasa linapokuja suala la kutoa huduma za fedha kwa waliokuwa hawahudumiwi vya kutosha. Sisi Visa, tunaamini kuwa uchumi wa kidigitali huongeza usawa na ukuaji wa pamoja, VEI in njia muhimu ya kuwasaidia wabunifu walio mstari wa mbele katika eneo hili,” aliongeza.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2015, VEI imezisaidia baiashara zinazoanza katika zaidi ya nchi 100 na kukusanya zaidi ya Dola za Marekani 16 bilioni (Sh36.8 trilioni) kwa ajili hiyo, ukuwa na mtandao wa biashara zinazoanza 12,000 duniani. Mwaka janaVEI iliwapa tuzo zenye thamani ya zaidi ya $530,000 katika mashindano hayo yaliyoshuhudia zaidi ya biashara 4,000 zinazoanza kutoka kanda tano zikishiriki. Mwaka jana, VEI ilishuhudia kampuni ya Nigeria ya ThriveAgric ikishinda tuzo kubwa ya VEI ya Dola za Marekani 100,000. ThriveAgric pia ilishinda Dola za Marekani 20,000 ya tuzo ya Visa Direct.

VEI inawalenga wavumbuzi na wajasiriamali wenye malengo makubwa wanaoziinua jamii kuwa kutatua changamoto za kufanya malipo na biashara zinazozikabili biashara katika sekta zote.

Mshindi wa jumla wa jumla wa dola 100,000, Ayo Arikawe (Katikati) kutoka kampuni ya Thrive Agic yw Nigeria akiwa jukwaani na Andrew Torre, (Kulia) Rais wa Mkoa wa Visa kwa Ulaya ya Kati na Mashariki, Mashariki ya Kati na Afrika (Visa Regional President for Central and Eastern Europe, Middle East and Africa (CEMEA) na Otto Williams, Makamu wa Rais Mwandamizi wa Visa, Mkuu wa Bidhaa, Ubia, na Suluhu za Kidijitali (Visa Senior Vice President, Head of Product, Partnerships, and Digital Solutions (CEMEA)wakati wa tuzo hizo nchini Dubai.
Mshindi wa mwaka jana - Ayo Arikawe (Kushoto) mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Thrive Agic ya Nigeria akipokea zawadi ya dolla 100,000 Dubai
Washindi katika tuzo mbalimbali mwaka jana wakiwa katika picha ya pamoja Dubai.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...