Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma
BOHARI
ya Dawa (MSD) imeanika hatua mbalimbali inazochukua kuondokana na
changamoto ya kuagiza vifaa tiba mbalimbali kutoka nje ikiwa pamoja na
kuanzisha viwanda viwili vya barokoa na kimoja cha kuzalisha mipira ya
mikono (groves).
Hayo
yamesemwa leo Aprili 6, 2023 na Hassan Ibrahimu kutoka Idara ya
Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji wa Bohari ya Dawa (MSD), alipokuwa
akielezea sababu za bohari hiyo kuanzisha kampuni tanzu na viwanda
vyake.
Akifafanua
zaidi wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini katika
semina iiyoandaliwa na MSD kuwajengea uwezo kuhusu shughuli za za
bohari hiyo, Ibrahim amesema moja ya kiwanda kinachomilikiwa na MSD ni
kinachozalisha barakoa kilichopo Keko jijini Dar es Salaam.
“Kiwanda
hicho kina uwezo wa kuzalisha barakoa 80 kwa dakika, uwekezaji wake ni
Sh. bilioni 1.4 ambacho kwa mwaka kinazalisha barakoa milioni 5.8
kilianza kazi Agosti 2020. Kiwanda hiki kinaonesha umuhimu wa viwanda,
kilianza kazi wakati wa janga la UVIKO-19 na wakati ule haikuwa rahisi
kupata barakoa.
“Barakoa
moja ilikuwa ikiuzwa sh. 1,600 lakini baada ya kiwanda kuja sasa
inauzwa Sh. 500, uwepo wa kiwanda hiki umesaidia kabisa kuacha kuagiza
nje, kwa maana hiyo kiwanda kimepunguza matumizi ya fedha za kigeni,”
amesema Ibrahim.
Pia,
amesema kiwanda kingine ni cha kuzalisha barakoa za N95 chenye uwezo wa
kuzalisha barakoa 100 hadi 150 kwa saa moja ambacho kimekamilika na
kuzinduliwa rasmi Machi mwkaa huu, ambapo MSD imepata kibali cha kuanza
usambazaji.
Aidha,
amesema kuna kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono (glove) kilichopo
Idofi mkoani Njombe na sasa kina uwezo wa kuzalisha glove 10,000 huku
akieleza kiwanda hicho kitaanza uzalishaji Julai 25 na kitakidhi
mahitaji kwa asilimia 100.
“Kiwanda
kitatoa ajira zaidi ya 200 za moja kwa moja na ambazo si za moja kwa
moja. Viwanda vyote hivyo vitaokoa fedha za kigeni na tunataka malighafi
za viwanda hivi zitoke nchini. Tukifanikwa tunaweza kutengeneza
mzunguko mzima na hivyo kuimarisha uchumi
Meneja
kutoka Idara ya Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji wa Bohari ya Dawa
(MSD) Hassan Ibrahimu akizungumza mbele kwenye Semina ya Wahariri wa
Vyombo vya habari nchini kuhusu hatua mbalimbali inazochukua kuondokana
na changamoto ya kuagiza vifaa tiba mbalimbali kutoka nje ikiwa pamoja
na kuanzisha viwanda viwili vya barokoa na kimoja cha kuzalisha mipira
ya mikono (groves).
Meneja
Mawasiliano na Uhusiano Bohari ya Dawa (MSD) Etty Kusiluka akitoa
maelekezo mbalimbali wakati wa semina ya siku mbili ya Wahariri wa
Vyombo habari nchini, jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF),Deodatus Balile (kulia) pamoja na
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bohari ya Dawa (MSD) Etty Kusiluka na
baadhi ya Wahariri wakifutilia wasilisho lililokuwa likihusu Mabadiliko
ya sheria ya MSD n Uanzishwaji wa kampuni Tanzu.Mweyekiti
wa Muda wa semina ya siku mbili ya Wahariri wa Vyombo habari
nchini,Mgaya Kingoba akitoa muongozo namna ya kufanya majadiliano
kufuatia mawasilisho yaliyokuwa yakiwasilishwa ukimbini humo.Pichani
kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai
akifuatilia.
Baadhi
ya Wafanyakazi waandamizi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakifuatilia mambo
mbalimbali yaliyokuwa yakiwasilishwa ukumbini humo wakati wa semina ya
Wahariri wa Vyombo vya habari ambayo imeratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD)
jijini Dodoma.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatlia yaliyokuwa yakiendelea kwenye semina hiyo.Picha zote na Michuzi Jr-MICHUZI MEDIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...