Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Liu Jianchao leo jijini Beijing nchini China.

Viongozi hao wawili walibadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa vyama na nchi hizo Novemba mwaka jana wakati wa Ziara ya Kiserikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini China. Pia walikubaliana kuimarisha mawasiliano na ushirikiano baina ya vyama, na kukuza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania.

Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo amewasili jijini Beijing nchini China kwa ziara ya kikazi akiwa ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa .












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...