Njombe

Wahitimu 34 wa mfunzo ya awali ya mpira wa miguu kwa watoto (Grassroots) wamehitimisha mafunzo ya siku tano ya ualimu wa watoto mkoani Njombe yaliyotolewa na shirikisho la mpira Tanzania (TFF) iliyohusisha washiriki mbali mbali kutoka halmashauri za mkoa huo.

Akifunga mafunzo hayo Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye pia ni mdau wa soka mkoani Njombe ametoa wito kwa wahitimu kutumia ujuzi walioupata ili kuinua kiwango cha soka na vipaji mkoani humo.

"Kozi hii ni muhimu sana kwa mustakabali na maendeleo ya soka ndani ya mkoa wetu wa Njombe na taifa kwa hiyo tusichukulie ni kitu kidogo tunapaswa kwenda kuwajibika"alisema Mpete

Aidha katibu wa Chama cha mpira mkoa wa Njombe (NJOREFA) Lucas Ndifua amesema baada ya Njombe mji kushuka daraja kwa sasa mkoa huo umejipanga kutengeneza timu nyingine itakayocheza ligi kuu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...