Na. Farida Ramadhani WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Mfumo wa Benkiwakala wa Bima umesaidia kukuza biashara ya Bima nchini.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini Mhe. Innocent Edward Kalogeris aliyetaka kujua kama Serikali haioni kuwa kuruhusu Benki kuwa Wakala wa Bima, Mawakala wengine watafunga biashara kwa kukosa wateja.

Mhe. Nchemba alisema Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na wadau wa bima ilianzisha Benkiwakala wa Bima ili kuongeza wigo wa usambazaji na upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi.

“Idadi ya Wakala wa Bima wa Kawaida imekuwa ikiongezeka sambamba na Benkiwakala wa Bima kwa sababu hali hii imechochea ushindani, ubunifu na kutegemeana”, alibainisha Mhe. Nchemba.

Alisema Takwimu zinaonesha Benkiwakala waliosajiliwa ni 14 (2020), 23 (2021), 27 (2022) na 30 hadi Machi 2023 huku Wakala wa Bima wa Kawaida waliosajiliwa ni 745 (2020), 789 (2021), 910 (2022) na 960 kati ya Julai 2022 na Machi 2023.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...