Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Mashaka Juma (kulia) akimpatia maelezo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Ernest Hinju (katikati) pamoja na Afisa Mkuu wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Jackson Shayo (kushoto), kuhusu namna kituo cha mawasiliano cha mfumo wa m-mama kitakavyorahisisha upatikanaji wa usafiri wa dharura ili kuokoa maisha ya wajawazito na Watoto wachanga. Uzinduzi wa huduma ya m-mama ulifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ikiwa ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania, Vodacom Tanzania Foundation, Pathfinder, Touch Foundation na USAID.


Afisa Mkuu wa TEHAMA kutoka Wizara ya Afya, Jackson Shayo akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Ernest Hinju, kuhusu namna kituo cha mawasiliano cha mfumo wa m-mama kitakavyorahisisha upatikanaji wa usafiri wa dharura ili kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na Watoto wachanga. Uzinduzi wa huduma ya m-mama ulifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ikiwa ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania, Vodacom Tanzania Foundation, Pathfinder, Touch Foundation na USAID.

Meneja wa m-mama kutoka taasisi ya Vodafone Foundation, Rahma Bajun akielezea kuhusu namna kituo cha mawasiliano cha mfumo wa m-mama kitakavyorahisisha upatikanaji wa usafiri wa dharura kuokoa maisha ya kina mama wajawazito na Watoto wachanga kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, Dkt. Darama Paschal (kushoto), Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Ernest Hinju (katikati), na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Mashaka Juma (kulia). Uzinduzi wa huduma ya m-mama ulifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ikiwa ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania, Vodacom Tanzania Foundation Pathfinder, Touch Foundation na USAID.


Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom Tanzania PLC Happiness Shuma akisikiliza namna ambavyo mfumo wa m-mama utaokoa maisha ya akina mama Wajawazito na Watoto Wachanga wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. Uzinduzi wa huduma ya m-mama ulifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ikiwa ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania, Vodacom Tanzania Foundation, Pathfinder, Touch Foundation na USAID.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...