Na Jane Edward, Arusha
Baraza la taifa na usimamizi wa mazingira NEMC limetoa miezi sita kwa wamiliki wa baa na kumbi za starehe pamoja na baadhi ya nyumba za starehe kote nchini yanayoendesha shughuli zao kwa kelele chafuzi majira ya usiku kuacha mara moja ndani ya kipindi hicho kwani serikali itaaza kuchukua hatua zidi yao.
Kauli hiyo imetolewa jijini Arusha na mkurugenzi mkuu wa NEMC nchini Dr.Samuel Gwamaka wakati alipotembelea moja ya kanisa lililopo mtaa wa Sama kata ya Moivo wilayani Arumeru linalotuhumiwa na wananchi kuendesha kelele chafunzi majira ya usiku bila kufuata sheria za mazingira.
Gwamaka amesema agizo hilo ni la miezi sita na ni kwa nchi zima kutekeleza sheria za mazingira na ndani ya kipindi hicho watakao kiuka tutawachukulia hatua ikiwemo kuwafungia hadi hapo watakapo kidhi vigezo vya mazingira.
"Sheria ziluzowekwa ni lazima ziheshimiwe kelele chafuzi zikiwepo zinasumbua wananchi wengine kwani kwenye jamii kuna watu mbalimbali ikiwemo wagonjwa"Alisema
Naye Mwenyekiti wa mtaa huo Baraka Shange pamoja na kupongeza juhudi za baraza la NEMC kufika katika mtaa huo amekiri kua hali ilikua mbaya ya kelele ambayo ilikua kero kwa wananchi wa maeneo hayo.
"sisi Kama wananchi wa mtaa huu tumekua tukilalamikia kelele ambazo zimekua zikizalishwa na kanisa hilo watu wanashindwa kulala nyakati za usiku lakini kwa sasa tunaimani kua ujio wa NEMC swala hili litamalizika"Alisema.
Mchungaji wa kanisa hilo Selestine Massawe pamoja na kupatiwa elimu ya mazingira na Baraza la Taifa na usimamizi wa mazingira Nemc ameahidi kufuata sheria pamoja na kutekeleza maagizo yote aliopatiwa na mkurugenzi mkuu wa Nemc.
"Nina ahidi kufuata maelekezo niliyopewa na NEMC ili kuweka mahusiano mazuri na jamii kwa kuwa natoa huduma za kimungu na migogoro haina afya "Alisema



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...