Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Gerson Msigwa amesema kuna umuhimu wa wahariri wa vyombo vya habari kukutana mara kwa mara na taasisi za umma.
Amesema lengo la kufanya hivyo ni kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kujenga uwelewa wa shughuli zinazotekelezwa na serikali pamoja na taasisi zake na mashirika hatua ambayo itasaidia kuwajengea uwelewa mpana zaidi.
Msigwa ameyasema hayo leo Aprili 5,2023 jijini Dodoma wakati akitoa salamu kwenye semina ya siku mbili iliyoanza leo ambayo imeratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.
“Tunawaomba wahariri wa vyombo vya habari nchini kuendelea kushirikiana na Serikali, tumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kuhusu kukutanisha wahariri na watendaji wa taasisi.
“Juzi tulikuwa na kikao kazi cha maofisa habari, moja ya jambo ambalo tumejifunza mwakani tutawaita wahariri wa habari, na tumepanga tuwe tunawakutanisha wahariri na taasisi zetu mara kwa mara.Tunafanya mabadiliko na tutaanza huo utamaduni wa kukutana,”amesema Msigwa.
Amesema MSD wameanza kukutana na wahariri lakini wataendelea kualikwa kwenye taasisi nyingine,lengo ni kuendelea kushirikiana huku akifafanua wakati mwingine kumekuwepo na upotoshaji kwasababu ya kukosa taarifa.
“Tukikutana na kuelimishana tutapunguza upotoshaji ambao umekuwa ukitokea , naamini tukiwa tunakutana tutapunguza.Niwapongeze wahariri kwa kuendelea kushirikiana na Serikali.
“Matatizo ya upotoshaji mengi hayatokei kwenye vyombo vya habari vikubwa bali mitandaoni na huko tunajua sababu zake.Nitoe rai kwenu wahariri wa vyombo vya habari linapotokea jambo tushirikishane.Kukiwa na jambo linahusu taasisi uliza.”
Aidha amesema Serikali itaendelea kufanya yale ambayo yamekuwa yakizungumzwa na sasa wanaendelea na suala la kufuatilia uchumi kwenye vyombo vya habari .Serikali haifurahishwi na hali ya uchumi wa vyombo vya habari.




Pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai pamoja na Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi wakifurahia jambo mara baada ya kumsikiliza Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Gerson Msigwa wakati akitoa salamu kwenye semina ya siku mbili iliyoanza leo ambayo imeratibiwa na Bohari ya Dawa (MSD) kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.




Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatlia yaliyokuwa yakiendelea kwenye semina hiyo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...