Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
BONDIA wa Ngumi za Kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo amewataja mabondia anaowakubali hapa nchini, mbali na bondia Tony Rashid, amewataja Juma Choki, Nasibu Ramadhan na Emmanuel Mwakyembe.

Mwakinyo anayepigana kwenye uzani wa Light Middleweight amewataja mabondia hao baada ya kuulizwa swali na mdau wa ngumi ambaye ni shabiki yake, baada ya kutoa nafasi ya kuulizwa maswali kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii (Instagram).

“Ni bondia yupi wa Tanzania ambaye unapenda aina yake ya uchezaji ulingoni ukiacha Tony Rashid?”, ameuliza mdau mmoja wa ngumi ambaye ni shabiki yake Hassan Mwakinyo.

Mwakinyo amejibu: “Juma Choki, Nasibu Ramadhan na Emmanuel Mwakyembe.”

Vile vile, Mwakinyo amekiri kukabiliwa na mpinzani bora kwenye pambano lake lijalo dhidi ya Bondia Kuvesa Katembo waAfrika Kusini huku akibainisha kuwa mabondia hao kutoka Afrika Kusini ni wazuri na bora kutokana na kupata mafunzo kutoka kwa Walimu wao (Coaches) wazuri.

Aprili 23, 2023 bondia Mwakinyo mwenye nyota mbili na nusu kwa sasa, atapanda ulingoni kupambana na mpinzani wake kutoka nchini Afrika Kusini, Kuvesa Katembo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma huku pambano hilo likitanguliwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo mapambano ya wabunge wa Bunge la Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...