Na Pamela Mollel,Arusha

Waziri wa Fedha na Mipango  Dkt. Mwigulu Nchemba ameipongeza Benki ya Mwanga Hakika kwa kuendelea kutoa huduma kwenye miradi ya miundombinu na kufanya kazi na wajasiriamali hapa nchini

Akizungumza jijini Arusha wakati akizindua tawi jipya na la kisasa lililopo katika jengo la central plaza, hafla iliyohudhuriwa na wafanyabiashara wakubwa kutoka Arusha na nje ya Arusha

Waziri Nchemba alisema kuwa jitihada za benki hiyo kujitanua ni fursa kubwa kwa wananchi wa kada mbalimbali kufikiwa na huduma za kifedha pamoja na kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu

Pia aliwataka wananchi kuwa na nidhamu ya mikopo kwani watu wengi wanakopa bila kujua wanafanyia nini kwa kuwa hawakujiandaa vizuri
"Watu wengi wanaomba fedha katika Taasisi mbalimbali za kifedha lakini hawana malengo kusudiwa "alisema Nchemba

Aidha alitoa rai kwa maafisa wa mabenki hapa nchini kuhakikisha kuwa kila mkopaji awe na lengo linaloeleweka ili aweze kurejesha fedha za mkopo kwa wakati

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Jagjit Singh alisema lengo la Taasisi hiyo ya fedha nikufanya iwe ya kimataifa zaidi

"Benki hii ilianzishwa mwaka 1998 ikiwa ni benki ya kijamii na mwaka 2020 ilikuwa ni benki ya Microfinance na mwaka 2022mpaka sasa ni benki ya biashara "alisema Singh

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Mwanga Hakika alisema benki hiyo imejitanua zaidi kuhudumia wateja wengi zaidi ambapo itatoa faida kwa wenye hisa na wateja wengine wa benki hiyo

"Mpaka sasa idadi ya matawi ya benki yapo saba mengine yapo Dar es Salaam,Moshi, Dodoma, Mwanga na Same.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...