Benki ya Exim Tanzania
imehitimisha rasmi zoezi la uandaaji wa futari kwa wateja wake katika
mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar, Dodoma na
Tanga kwa msimu huu wa mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani huku wadau
mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo wateja, viongozi wa dini na serikali
wakionyesha kuridhishwa na utaratibu wa benki hiyo wa kuwakumbuka watu
wenye mahitaji maalum katika mwezi huo.
Katika kuhitimisha zoezi
hilo ilishuhudiwa viongozi waandamizi wa serikali na dini katika mikoa
ya Tanga na Dodoma wakishirikiana na viongozi waandamizi wa benki hiyo
akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu Bw Jaffari Matundu pamoja na Mkuu wa
Rasilimali watu wa Benki hiyo Bw Fredrick Kanga katika kuongoza hafla
mbili tofauti zilizoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake
wenye imani ya Kiislam katika mikoa hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Sambamba
na hafla hizo benki hiyo pia kupitia Mkuu wake wa kitengo cha Hazina
na Masoko ya Dunia Bw Nelson Kishanda pamoja na baadhi ya wateja wake
iliweza kukabidhi msaada wa chakula na mahitaji muhimu kwa familia
zenye uhitaji kupitia taasisi ya Maawal Islamic ya jijini Tanga, zoezi
ambalo liliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa
aliemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, sambamba na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo
Sheikh Juma Luwuchu.
Wakizungumza kwenye matukio yote mawili ya
jijini Tanga DC Mgandilwa pamoja nae Sheikh Luwuchu walionyesha
kufuruhishwa na mtazamo wa benki hiyo wa kutokutazama mwezi wa Ramadhani
kama ni mwezi wa kujenga mahusiano na wateja wao pekee bali pia
kuutumia vyema mwezi huo kwa kuyakumbuka makundi yenye uhitaji bila
kujali kama si wateja wa benki hiyo.
“Hiki kinachofanywa na
benki ya Exim ni mfano haswa wa kuigwa. Wangeweza tu kukutana na wateja
wao na kufuturu pamoja lakini wameona kitendo hicho pekee hakitoshi
kuuheshimisha mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani hivyo wameona ni vema
wawakumbuke pia wenye uhitaji maalum. Kupitia Taasisi ya Maawal Islamic
wameweza kukabidhi futari kwa watu wenye uhitaji…hongereni sana,’’
alipongeza DC Mgandilwa.
Akizungumzia matukio hayo Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alisema ni muendelezo
wa utaratibu wa benki hiyo kwa zaidi ya10 miaka sasa ikilenga kujumuika
na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika
kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Alisema benki hiyo
inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni
kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia
mfungo na kufanya maombi.
“Kwetu sisi mwezi huu tunautazama
kiimani zaidi ndio sababu tunazama makundi yote wakiwemo wateja wetu
pamoja na watu wenye uhitaji maalum. Tumeweza kuandaa matukio kama haya
mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar na leo tunakamilisha na
mikoa ya Tanga na Dodoma.’’
“ Zaidi tutaendelea kutoa zawadi za
Sikukuu ya Eid al-Fitr katika maeneo mengine pia. Lengo ni wote
tufurahie mwezi huu muhimu huku pia tukikumbushana kufanya kilicho chema
mbele za Mungu wetu.” Alisema Matundu.
Hafla zote mbili
zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali,
viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja
na wafanyakazi wa benki hiyo.
Maofisa
wa Benki ya Exim Tanzania akiwemo Mkuu wa kitengo cha Hazina na Masoko
ya Dunia Bw Nelson Kishanda (katikati) wakikabidhi msaada wa chakula
na mahitaji muhimu kwa mmoja wa wananchi wenye uhitaji jijini Tanga
ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na
wateja wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Wanaoshuhudia
ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa (wa tatu
kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luwuchu (kushoto)
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu ( wa tatu kushoto)
sambamba na wageni waalikwa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim
Mgandilwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luwuchu wakipata
futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili
ya wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Hafla
zote mbili zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa
serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja,
mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Tanga Bw Hashim Mgandilwa (wan ne kushoto) na Sheikh Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Sheikh Juma Luwuchu (katikati) wakiwa kwenye picha ya
pamoja na wafanyakazi pamoja na wateja wa benki ya Exim wakiongozwa na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu ( wan ne kulia)
wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya
wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza na wageni
waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa
ajili ya wateja wake jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Rasilimali watu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Fredrick Kanga
akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa
na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed abbas akitoa neno la shukrani kwa niaba
ya wageni wengine waalikwa waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa
na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma
mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakipata futari wakati hafla ya futari iliyoandaliwa
na benki ya Exim Tanzania kwa ajili ya wateja wake jijini Dodoma
mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa kitengo cha Hazina na Masoko ya Dunia Bw Nelson Kishanda
(alisimama) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa
chakula na mahitaji muhimu kwa wananchi wenye uhitaji jijini Tanga ikiwa
ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuwa karibu zaidi na wateja
wake katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Home
HABARI
Benki ya Exim Yaandaa Hafla ya Futari Dodoma na Tanga, Viongozi wa Dini, Serikali Waguswa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...