Na Mwandishi Wetu,Same

KAMATI ya Usalama Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro imeamua kuingilia kati na kusitisha mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Empower Tanzania kwa walimu wa shule za msingi na Sekondari wilayani humo baada ya kubaini mafunzo hyo yanaviashiria vya maadili yasiyofaa.

Mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo yalikuwa yanahusu afya ya jamii , afya ya uzazi na mahusiano lakini Kamati ya ulinzi na usalama imebaini uwepo wa viashiria amnavyo haviendani na maadili ya Mtanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesema katika ufuatiliaji wamebaini kuna upungufu mkubwa ikiwemo baadhi ya picha na maneno yaliyomo kwenye vitabu vinavyotumiwa na taasisi hiyo kufundishia kuwa na viashiria vya kuhamasisha mambo yasiyo faa kwa wanafunzi.

Mbali na kusitisha mafunzo,pia Kamati ya ulinzi na usalama imemtaka Mkurugenzi wa taasisi hiyo kusitisha shughuli zote zinazohusu mafunzo ya afya ya jamii,afya ya uzazi na uhusiano kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Same mpaka itakapoamriwa vinginevyo.Mkurugenzi huyo kusaidia vyombo vya usalama kutoa ufafanuzi wa masuala hayo.

Mgeni amesema kwamba vitabu vilivyobainika kutumiwa na taasisi hiyo huenda ni kati ya vile vilivyotolewa katazo na Serikali kutosambazwa wala kutumiwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini hasa kwenye taasisi za elimu na kwamba vitabu vyote vichukuliwe kwa ajili ya uchunguzi zaidi, pia kufanyiwa marekebisho kabla ya kutumika kama itafaa.

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Kasilda Mgeni akizungumza wakati wa kikao Cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kilichotoa uamuzi wa kusitisha mafunzo ya Taasisi hiyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...