Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma
MFAMASIA Mkuu wa Serikali Daud Msasi amewahakikishia Watanzania kwamba dawa zinazozalishwa nchini zimethibitishwa na zina ubora unaostahili.
Msasi ametoa maelezo hayo kwenye semina kwa wahariri wa habari nchini iliyoandaliwa na MSD ambapo baadhi ya wahariri walitaka kufahamu ubora wa dawa zinazozalishwa nchini iwapo zina ubora sawa na zile zinazotoka nje ya Tanzania.
“Dawa zetu ni bora, ila tiba ni pamoja na mtazamo, unakunywa dawa halafu unasema hata nikinywa siponi. Niwahakikishie dawa zetu zina ubora unaostahili na zimethibitishwa.
“Familia yangu tunakunywa dawa za Tanzania na sababu TMDA yuko nyumbani, anaweza kukagua mara kwa mara. Dawa zote tunazokunywa zimethibitishwa na TMDA ambayo kwa ubora Afrika ni ya kwanza, hivyo dawa zetu zinaweza kwenda hata Marekani,” amesema Msasi.
Akijibu swali kuhusu idadi ya viwanda vya dawa na vifaa tiba vilivyopo nchini, Mfamasia Mkuu wa Serikali alisema kwa sasa kuna viwanda 11 vinavyozalisha dawa na 24 vya vifaa tiba, hivyo jumla vipo viwanda 35.
Hata hivyo, alisema bohari ya dawa inajitahidi kuhakikisha huduma zake hazisimami kwani hilo likitokea husababisha athari ambazo huonekana baada ya muda.
“Matokeo yanakuja baada ya miezi 12 mzima, sifuri (kukatika kwa mnyororo wa usambazaji) mwaka 2019/2020 matokeo yakaja 2022,” amesema.
Amesema kazi kubwa imeendelea kufanyika na sasa ukienda malalamiko ya ya upungufu au kukosekana kwa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya yamepungua.
Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi akizungumza jijini Dodoma wakati akieleza kuhusu ubora wa dawa zinazozalishwa nchini kwenye semina ya Wahariri wa Vyombo vya hababri ya siku mbili,ambayo iliyoratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD).Picha na Michuzi Jr-MICHUZI MEDIA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...