Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Ni ukweli Mnyama, Simba SC ana safari ngumu na si nyepesi kufuzu Nusu Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAFCL) baada ya kupangwa na timu ya Bingwa mtetezi Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo.
Katika droo ya Michuano ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) ngazi ya vilabu iliyofanyika jijini Cairo nchini Misri, Simba SC amepangwa kucheza dhidi ya Wydad Casablanca, kabla ya hapo kulikuwa na uwezekano wa kucheza dhidi ya Mamelodi Sundowns au Esperance de Tunis.
Ni safari ngumu kwa Simba SC kwa sababu Wydad wana rekodi nzuri katika Michuano hiyo sanjari na kufanya vizuri zaidi katika Kundi lao wakati wa hatua ya makundi, sanjari na kufanya vizuri katika mashindano yao ya nyumbani nchini Morocco.
Wydad walikuwa Kundi A lenye timu za JS Kabylie ya Algeria, AS Vita ya DR Congo na Petro de Luanda ya Angola. Simba SC walikuwa Kundi C lenye timu za Raja Casablanca ya Morocco, Horoya AC ya Guinea na Vipers SC ya Uganda.
Simba SC wataanza hatua hiyo ya Robo Fainali wakiwa nyumbani na watacheza kati ya Aprili, 21-22, 2023 wakati mchezo wa mkondo wa pili watacheza kati ya Aprili 28-29, 2023.
Endapo, Simba SC watafuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo watacheza dhidi ya mshindi kati CR Belouizdad ya Algeria au Mamelodi Sundowns (Masandawana) ya Afrika Kusini.
KILA LA KHERI TANZANIA, KILA LA KHERI SIMBA SC KWENYE MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...