NA FARIDA MANGUBE.

Katika kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri mahala pa kazi Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) kimewakutanisha wafanyakazi wake kwenye hafla ya Iftar iliyonyika katika ukumbi wa Freedom Square uliopo Kampasi ya Solomon Mahlangu.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Prof. Raphael Chibunda amesema Chuo kimekuwa na desturi ya kufuturu pamoja na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

“Mara zote tumekuwa tukifanyia hafla hii katika Kampasi ya Edward Moringe, mwaka huu tumeamua kuandaa hafla hii Kampasi hii ya Solomon Mahlangu ni washukuru Waislamu na wote mliohudhuria katika Iftar ya leo mmetuheshimisha sana kwa kuacha shughuli zenu nyingi na kujumuika nasi.” Alisema Prof. Chibunda.

Aidha amewataka wafanyakazi kuendelea kuishi kwa umoja na upendo kama wanavyoishi katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na kwamba mwezi utakapomalizika kuendeleza yote yaliyo mema ikiwa ni pamoja na kwenye maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Mussa Ally Mussa akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Bi. Fatma Mwassa amesema ni vyema Taasisi kukutanisha wafanyakazi ili kudumisha umoja baina yao.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu  cha Sokoine cha kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda akizungumza kwenye hafla ya Iftari iliyofanyika  katika ukumbi wa Freedom Square uliopo Kampasi ya Solomon Mahlangu Mjini Morogoro.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa kwenye Hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ( SUA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...