Mwanafunzi wa Kitanzania kutoka Chuo cha US Berkeley anaamini kuwekeza katika uwezeshaji wa wanawake vijana kiuchumi kupitia NGO yake ya FEET Tanzania.
Taasisi ya Educational and Environmental Advancement of Tanzanians (FEET) imezindua Kambi maalum ya ujasiriamali kwa wasichana (GEC) yenye nia ya kutoa ujuzi unaohitajika ili kuongeze kiwango cha ufaulu shuleni, nyumbani na hata kwa taaluma za baadae kwenye maisha.
Programu hii imekuwa ikiendelea tangu Agosti mwaka jana na wikendi hii ya Pasaka ilifanyika kwenye shule ya sekondari ya AHMES iliyopo wilayani Bagamoyo.
GEC ilitengenezwa na mwanafunzi Mtanzania Rania Nasser, ambaye pia ni mwanafunzi katika ya shule ya Sekondari ya UC Berkeley na ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa taasisi ya FEET ili kuwatayarisha wasichana wenye umri kati ya miaka 14 na 18 ya kuwa wajasiriamali na kuwafundisha jinsi ya kuanzisha na kuendesha biashara.

Programu hii uchukua siku tau, wakati ambapo washiriki hufanya kazi katika timu na kufundishwa na waalimu wabobezi kwenye masuala ya ujasiriamali. Kwenye siku ya tatu, wanafunzi hawa uwasilisha na kutetea suluhisho lao kwenye jopo la waalimu. Mmoja wa wanafunzi walioshiriki kwenye programu hii Sarah Magomba alisema, ‘Kwa sasa najiamini sana, sasa najua jinsi ya kufanya mambo yafanyike na kuleta mawazo yangu kuwa halisi’.
‘Kwakuwezesha wanawake na vijana kwenye elimu na ujuzi kutawafanya waweze kuondokana na vikwazo vinavyowakabili na kuboresha hali zao za kiuchumi na kijamii’, alisema Rania Nasser.
Programu hii uanza na kuteua timu kwenye siku ya kwanza halafu ufuata mfululizo wa shughuli zinazowapa wanafunzi fursa ya kujifunza ujuzi na mambo mbalimbali, uwezo na haiba ya timu ya washiriki wenzao. Wanafunzi kisha hujifunza jinsi makampuni yanapotengeneza na bidhaa maalum na ambazo watu walengwa watazipenda au wanapenda. Kisha ufanya mazoezi ya uundaji wa bidhaa kwa kutumia dhana tatu asilia zinazotatua changamoto.
Siku ya tatu, washiriki hujifunza jinsi ya kupata na kutoa maoni, kuchukua wazo zuri kutoka kwenye dhana hadi muundo ulio tayari kwa bidhaa kuingia sokoni, na kutengeneza mkakati wa uuzaji ili kueneza ujumbe wa bidhaa mpya. Vile vile, hujifunza jinsi ya usimamizi wa masuala ya kifedha kupitia michezo ya kufurahisha na kuunda mpango wa bei na mpango wa kifedha na timu zao.
Kufikia mwisho wa programu, kila timu itakuwa imeandika mpango wa biashara na kufanya kazi ya kibunifu ili kuibua bidhaa zao. Washiriki watakuwa wamepata ujuzi muhimu, ikiwa ni pamoja na uongozi, kutatua migogoro, kuunda timu ya biashara, kuamua uwezekano wa biashara, kufanya utafiti wa soko, kuamua bei ya bidhaa, kufanya tathmini ya gharama, maendeleo na mapendekezo ya biashara, bajeti, udhibiti wa hesabu, masoko pamoja na kuwasilisha mawazo yao.
Akizungumzia kuhusu programu hii, Mkuu wa shule ya AHMES alisema mbinu ya programu ni ya kushughulikia, kuruhusu washirika washiriki kufanya mazoezi wanayojifunza na kuunda mpango wa biashara na bidhaa.
Akizungumza kuhusu programu hii, Mkuu wa shule ya AHMES alisema mbinu ya programu hii ni ya kushughulikia, kuruhusu washiriki kufanya mazoezi wanayojifunza na kuunda mpango wa biashara na bidhaa ifikapo mwisho. Mbinu hii husaidia kujenga kujiamini na kujitengemea, ambayo ni muhimu kwa wanawake vijana kufanikiwa kama wajasiriamali. Programu hii inaleta hamasa kwa kutambua kuwa imekuwa ikiendelea tangu Agosti 22 na mpaka sasa shule 51 zimenufaika.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya AHMES wakiwa tayari kuwasilisha suluhisho kwa walimu kwenye kambi maalum ya GEC iliyoandaliwa na FEET.

Wanafunzi wasichana wa sekondari wakifurahia katika moja ya kambi ya GEC iliyoandaliwa na FEET Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...