Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo tarehe 18/4/2023 imekabidhi vifaa vya kielektroniki kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning Improvement Cooperation 2022) pamoja na uzinduzi wa maabara ya TEHAMA kwa shule ya Msingi Tegeta "A" ya jijini Dar es salaam.

KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia ya mtandao kwa walimu 20 wa shule ya msingi Tegeta A.

Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET , Dkt. Aneth Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hiyo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya ufundishaji na ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.

Dkt Komba amewataka walimu hao kuhakikisha wanaleta matokeo chanya ambayo yatasaidia katika uboreshaji wa elimu.

"Mkayatumie mafunzo vizuri na vifaa hivyo mlivyokabidhiwa kwa kuleta matokeo chanya na tuone ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Tegeta A" ,Amesema Dkt.Komba.

Tukio hilo liliambatana na kukabidhi vishikwambi 20 kwa walimu walioshiriki programu ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake , Mwalimu Mkuu wa shule ya Tegeta A Bwana. Alistides Ntakire ameshukuru kwa mafunzo hayo pamoja na vifaa vilivyotolewa ambapo amesema ana imani yataleta tija katika shule yake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Bwana Yassin Marijan ameshukuru kwa kuzinduliwa maabara hiyo ya TEHAMA na kukabidhiwa vifaa vyote huku akieleza kuwa atahakikisha vinatumika ipasavyo katika kuboresha elimu.

Vifaa vilivyokabihiwa ni pamoja na 'UPS 26,computure Monitor 25, system Unit 25,Wirless keyboard 35,projector moja, scanner moja,printer moja, wireless mouse 35, headphone 25, electric blackboard moja ,webcamera 26,digital podium moja,wired keyboard 25, ,wired mouse 25,speaker 26,adapter 49 na usb flash disk 50'
Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Maabara ya TEHAMA katika shule ya Msingi Tegeta A, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Yassin Marjan. Tukio lililofanyika leo Aprili 18, 2023.
Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akiwa anavitoa kuwakabidhi vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 uongozi wa shule ya Tegeta A, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala, Dkt. Fika Mwakabungu. Tukio hilo lililofanyika mapema leo Aprili 18, 2023.
Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba Akizungumza katika tukio hilo la ukabidhaji wa vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 na uzinduziwaMaabaraya TEHAMA. mapema Aprili 18, 2023.
Baaadhi Walimu wa shule ya Msingi Tegeta A,  wakiwa wamebeba vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022, mapema leo Aprili 18, 2023.
Mkrugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt.Aneth Komba akikamkabidhi  Mwalimu Mkuu wa shule ya Tegeta A, Mwl. Alistides Ntakire vifaa vya kielektroniki vilivyotelewa na Korea kupitia mradi wa KLIC 2022.  Tukio lililofanyika leo Aprili 18,2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...