Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amemuagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wajasiriamali wapya hawatozwi kodi kabla ya kuanza kufanya biashara.
Mhe. Chande ametoa agizo hilo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, alipotaka kujua ni lini Serikali itaona haja ya kuondoa malipo ya kodi kwa wajasiriamali kabla ya kuanza rasmi kufanya biashara.
Mhe. Chande alisema kuwa Serikali kupitia Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019, Kifungu cha 43 imetoa unafuu wa kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita kwa biashara mpya tangu muhusika anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi, lengo likiwa kumpa mjasiriamali nafasi ya kustawi kibiashara.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, kuhusu malipo ya Kodi kwa Wajasiriamali kabla ya kuanza rasmi kufanya biashara.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...