Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma
BOHARI ya Dawa (MSD) imesema ipo katika hatua za mwisho kusajili kampuni tanzu ya kusimamia uzalishaji wa bidhaa ambayo itaendeshwa kibiashara.
Hayo yamesemwa leo Aprili 5, 2023 na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini ambao wamehudhuria semina ya kuwajengea uwezo na kubadilishana uzoefu inayoendelea jijini Dodoma.
“Katika moja ya eneo ambalo tunasema tumepata mafanikio ni pamoja na uzalishaji bidhaa , na hapa tunasema kwa sauti kubwa.MSD inaviwanda vyake, kiwanda cha Idofi ambacho kinatengeneza glove lakini tunacho , kiwanda cha kutengeneza Maski ambacho kipo Keko.
“Kwenye uzalishaji tulitafakari tukaona tukichukua jukumu kama lilivyo hatutaweza, tukaamua tutafute njia, tukaanzisha kampuni tanzu, tayari iko hatua za usajili na itakuwa inauza bidhaa zake kwa MSD. Tumeiruhusu MSD ijiendeshe kibiashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai akizungumza leo Aprili 5,2023
jijini Dodoma wakati akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Bohari ya Dawa kwenye semina ya siku mbili iliyoanza
leo ambayo imeratibiwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa wahariri wa vyombo
vya habari nchini



Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya habari wakifuatlia yaliyokuwa yakiendelea kwenye semina hiyo

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Bohari ya Dawa (MSD) Eti Kusiluka akitoa maelekezo mafupi kabla ya kuanza kwa semina ya siku mbili ya Wahariri wa Vyombo habari nchini leo Aprili 5,2023 jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...