Na Humphrey Shao,Michuzi Tv

WAKALA wa Barabara Tanzania( TANROADS) umesema ujenzi wa daraja kubwa la Kidatu- Ifakara mkoani Morogoro umefikia asilimia 78 na kwamba ujenzi huo unatarajia kukamilika Oktoba mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amefafanua gharama za ujenzi wa daraja hilo ni Sh.bilioni 105.

"Mradio huu ni miongoni mwa miradi ya miundombinu inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini na Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia TANROADS,"amesema na kuongeza kukamilika kwa daraja hilo kutasaidia katika shughuli za uchukuzi kwa wakazi wa Malinyi ,Ifakara Kilombero kulekea Morogoro mjini na mikoa ya jirani.

Amefafanua awali kwenye eneo hilo kulikuwa ba daraja la chuma ambalo linapitisha gari moja moja hali iliyolazimu watu kusubiriana lakini daraja jipya litakapokamilika magari mawili yapita kwa wakati mmoja kwa kupishana kama ilivyo kwenye barabara za kawaida.

Mhandisi Kyamba pia akaelezea miradi iliyokwishakamilika ni mradi wa Kingolwila na Mikumi pamoja na Ihovi ambao ulikuwa ni kurekebisha maeneo korofi huku akiongeza kuwa kuna miradi mingine mitano inayoenda kutekelezwa kwenye Mkoa huo kwa mwaka huu."Tayari Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alikwishatoa fedha za kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo."
.
Picha ya Juu ikionyesha ujenzi  unavyoendelea  kwenye  Daraja hilo
Sehemu ya Nguzo  ambazo zimesimamishwa katika  eneo la Kilombero kwenye Mto Ruaha Mkuu ambapo Daraja linalojengwa hapo litasidia kuunganisha eneo la Kilombero na Ifakara.
Sehemu  ya Vyuma ambayo  vinataraji kutandikwa juu ya Daraja hilo kama vinavyoonekana katika picha.


Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba akizungumza na Waandishi wa habari eneo linalojengwa Daraja kubwa kuvuka Mto Ruaha Mkuu Kilombero Mkoani  Morogoro
Sehemu ya Nguzo  ambazo zimesimamishwa katika  eneo la Kilombero kwenye Mto Ruaha Mkuu ambapo Daraja linalojengwa hapo litasidia kuunganisha eneo la Kilombero na Ifakara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...