Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye (Mb) ameshiriki katika kukimbiza mbio za Mwenge wa Uhuru Tarehe 11 Aprili, 2023 katika Hamashauri ya Mtama Mkoani Lindi.

Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zinazoongozwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Ndg. Abdullah Shaib Kaim, zimetembelea na kuweka jiwe la msingi kwa miradi inayoendelea kujengwa pamoja na kuzindua  miradi mingine mbalimbali Wilayani humo  ikiwemo mradi wa Mfumo wa TEHAMA katika Hospitali ya Nyangao, Mradi wa Utunzaji wa Misitu na Uhifadhi wa Mazingira, Mradi wa Usafirishaji Abiria, Mradi wa Barabara pamoja na Mradi wa Uboreshaji Miundomninu ya Maji-Mtama.

Mwenge wa Uhuru upo Wilaya ya Mtama na kesho utapokelewa na kikimbizwa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

#MwengewaUhuru #KaziIendelee #Mtama #Nape















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...