Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo ameendelea na ziara kikazi nchini China huku akiongozana na viongozi wengine wa CCM, wakiwemo Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC, Wenyeviti wa Mkoa pamoja na Wenyeviti wa Jumuiya.
Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM inalengo la kuendeleza mahusiano ya Kirafiki na Kindugu yaliyopo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kikomonisti Cha China (CPC).
Pamoja na Mambo Mengine CCM na CPC zimejikita zaidi katika kusaidiana katika mambo ya Elimu na Mafunzo ya Falsafa ya Siasa na Uchumi. Mahusiano kati ya vyama hivi, yameasisiwa na waanzilishi wa vyama hivyo vikongwe na kuendelea kuimarishwa na viongozi wa sasa.
Ziara hii imeanza tarehe 16 Aprili, 2023 na inatarajiwa kumalizika tarehe 26 Aprili, 2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...