Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imezindua rasmi usajili kwa ajili ya washiriki wa kongamano la usalama wa chakula litakalofanyika mwaka huu 2024 septemba 4 mpaka 8 Jijini Dar es salaam.


Uzinduzi huo umefanywa jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe mbele ya waandishi wa habari

Waziri Bashe amesema kongamano hilo litaangazia nafasi ya Bara la Afrika katika matumizi ya mbinu bunifu zitakazohakikisha Dunia inakuwa na usalama wa chakula.

Katika hatua nyingine Waziri Bashe amewaalika wadau wa Kilimo wakiwemo wataalamu wa masuala ya mifumo ya chakula Duniani.

"Wakati tukiendelea na jitihada za kuliwezesha Bara la Afrika kuwa kitovu cha usalama wa chakula Duniani, tunapaswa kuwapa kipaumbele vijana na wanawake katika harakati hizi' - Amesema Bashe.

Aidha amesisitiza umuhimu na nafasi ya viongozi wa Afrika katika kuchangia uwepo wa usalama wa chakula ngazi za Taifa na Bara huku akisisitizia ushiriki kwa vijana na wanawake.

Hata hivyo Bashe amesema kuwa mkutano wa AGRF mwaka huu utafungua milango ya matumizi ya ubunifu katika kuimarisha Kilimo pamoja na kufungua milango ya uwekezaji zaidi itakayohakikisha uwepo wa ubunifu, utugwaji wa sera Bora pamoja na uwekezaji kwenye Sekta ya Kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji WA jukwaa hilo Amath Pathe Sene amesemae kuwa ubunifu, Sera bora, uwekezaji wa kimkakati ni njia sahihi katika kuhakikisha upatikanaji wa mifumo imara ya chakula.

"AGRF 2023 itahusisha programu mbalimbali Kati ya wadau ambapo watapata wasaha wa kujadiliana na kubadilishana uzoefu" - amesema Amath.

Mkurugenzi huyo pia amesema septemba 3,2023 wagenj wa mkutano watapata wasaha wa kutembelea na kijionea shughuli za kilimo zinazofanywa na watanzania na kujioneae mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...