

Kampeni ya "Shinda Mechi Zako na NBC", inalenga kuongeza thamani kwa wateja wa NBC na kukuza ukuaji wao wa kifedha na uchumi wa nchi. Kampeni ina lengo la kuwafikia wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo, mawakala, na wengine wanaotumia huduma za benki za kimtandao kupitia NBC.Hafla ya uzinduzi huu umefanyika jijini Dar es salaam.[/caption] 3, MEI, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imezindua kampeni mpya inayojulikana kama "Shinda Mechi Zako na NBC".
Kampeni ya "Shinda Mechi Zako na NBC", inalenga kuongeza thamani kwa wateja wa NBC na kukuza ukuaji wao wa kifedha na uchumi wa nchi. Kampeni ina lengo la kuwafikia wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo, mawakala, na wengine wanaotumia huduma za benki za kimtandao kupitia NBC. Kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wa kada mbali mbali, Benki ya NBC imepanga kuwasaidia kutatua changamoto hizo kupitia ushauri na huduma za kifedha ambazo ni suluhisho za changamoito hizo na mechi na hivyo kuja na jina “Shinda mechi zako na NBC”,

Wateja pia wanaweza kupata mkopo wa kumalizia nyumba kwa gharama nafuu ili kukamilisha ndoto zao za ujenzi wa nyumba. Kampeni ya "Shinda Mechi Zako na NBC" inalenga kuimarisha ustawi wa kifedha wa wateja wa NBC na kusaidia juhudi za serikali katika kutoa huduma za kifedha, kukuza uchumi wa watanzania. NBC inaamini kuwa kampeni hii itawapa wateja faida kubwa na kuboresha thamani na uzoefu wa benki yao.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,, Mkuu wa Bidhaa za NBC, Abel Kaseko alisema, "Tuna furaha kuzindua kampeni ya 'Shinda Mechi Zako na NBC', ambayo ipo kwa ajili ya kuwapa nguvu wateja wetu na kuwasaidia kufikia malengo yao ya kifedha kwa kuongeza thamani na uzoefu wao wa benki. Kampeni hii itawapa wateja wetu huduma za KIbenki zenye gharama nafuu na rahisi, na pia kusaidia kukuza uchumi wao."




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...