Na Immaculate Makilika – MAELEZO
Serikali imedhamiria uchimbaji wa madini wa aina zote utumie umeme ili uwe na tija hivyo kuwawezesha wachimbaji kulipa tozo stahiki na kutoa gawio kwa Serikali.
Ambapo uwepo wa umeme katika mgodi wa Stamigold utasaidia kuokoa takribani shilingi milioni 700 kwa mwezi ambazo hutumika kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo na matarajio ni kushuka kwa kiwango hicho hadi shilingi milioni 300.
Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano maalum, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Mhe. ACP Advera Bulimba alisema kuwa anamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa shilingi bilioni 15.9 zilizowekezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) katika mgodi wa Stamigold ili kuweza kuwasha umeme katika mgodi huo.
“Niwaombe pia wafanyabiashara wengine waje kuwekeza Biharamulo kwa kuwa kwa sasa tunao umeme wa kutosha na mwingi”, alisema Mhe. Bulimba.
Kwa upande wake, Meneje Mradi kutoka TANESCO, Mhandisi Dismas Massawe anasema kuwa TANESCO wameendelea kujenga miradi mbalimbali ya kuunganisha wateja wakubwa hususan kwenye migodi.
“Mradi huu ulianza kutekelezwa rasmi Agosti 2020 baada ya kukamilisha ujenzi wa mradi wa kuunganisha umeme katika mgodi wa Stamigold, sasa hivi Shirika linawekeza nguvu zake na linaenda kukamilisha mradi wa kuweka umeme katika mgosi wa GGM” alisema Mhandisi Massawe.
Kwa upande wake, Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Kagera, Mhandisi Godlove Mathayo anasema “Mradi ulikamilika Aprili 20, 2023 na STAMIGOLD kuanza rasmi kutumia umeme wa gridiyaTaifa Aprili 26, 2023. Njia ya umeme iliyojengwa ni ya ukubwa wa kilovoti 33 ambayo ni ya umbali wa kilometa 105 kutoka kituo cha kupokea umeme cha Mpomvu – Geita” Alisema Mhandisi Mathayo.
Aidha, ujenzi umehusisha njia ya kusafirisha umeme pamoja na kituo cha kupokea na kupoza umeme cha STAMIGOLD. Kituo kimejengwa kwa transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 10 kila moja, na transfoma mbili za MVA 2.5.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...