Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa elimu kwa wadau wa uwekezaji na baadhi ya Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini juu ya Usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara lengo likiwa ni kuwahamasisha juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara.

Katika semina hiyo iliyofanyika leo tarehe 12 Mei, 2023 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam, Afisa Usajili kutoka BRELA, Bw. Greyson Moshi amewaelimisha wadau hao juu ya umuhimu wa urasimishaji wa biashara na kuwaeleza taratibu za kusajili kampuni na majina ya.Biashara.

Bw. Greyson amezitaja aina tatu za kampuni zinazosajiliwa BRELA kuwa ni Kampuni za nje (Foreign Company), Kampuni binafsi (Private Company), na Kampuni za Umma (Public Company), sambamba na kueleza taratibu za usajili wa kampuni ambao unafanyika kwa njia ya mtandao wa (ORS) unaopatikana katika tovuti ya BRELA kupitia www.brela.go.tz

Semina hiyo imehudhuriwa na wadau wa uwekezaji, watu binafsi wenye kampuni na wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA).

Mwenyekiti wa Umoja wa Uwekezaji na Wajasiriamali nchini Bw. Sebastian Kingu amewasisitiza vijana kutumia fursa ya kujiunga katika umoja ili kufungua kampuni zao binafsi zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi na kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na tekinolojia.

Semina hiyo iliyondaliwa na Umoja wa Uwekezaji na Wajasiriamali nchini Tanzania ilihusu fursa za Vijana kujiunga na kufungua makampuni binafsi ili kujikwamua na changamoto za ajira nchini, sambamba na kuendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Tekinolojia.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...