…. Wanafunzi 150 kufaidika na ujuzi wa kisasa wa teknolojia ya viyoyozi

Daikin, moja ya makampuni yanayoongoza katika teknolojia ya kisasa ya viyoyozi duniani, imeshirikiana na Chuo cha Ufundi cha Don Bosco Tanzania kuanzisha kituo cha kisasa cha ufanisi (centre for excellence) chenye mitambo yenye thamani ya zaidi ya $10,000 (Tshs. 235.5 milioni) itakayotumika kuwafundsiha wanafunzi kuhusu teknolojia ya kisasa ya viyoyozi.

Mpango huu, ambao umelenga wanafunzi 150 kwa kuanzia, ni sehemu ya Daikin kurudisha kwa jamii. Mradi huo pia unalenga katika utunzaji wa mazingira kama namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wanafunzi watapata ujuzi wa namna ya kukabiliana na joto, hewa safi na viyoyozi (HVAC) huku wakitumia teknolojia ya hali ya juu kutoka Daikin, inayohusisha mitambo maalumu ya kisasa ijulikanayo kama, Variant Refrigerant Volume (VRV), inverter, heat pump, na mashine za jokofu yaani refrigerant machines.

Wanafunzi hao watapata mafunzo mbalimbali ili kuwafanya wawe na maarifa zaidi kaika nyanja ya HVAC. Hii ni pamoja na ukaguzi wa jumla, matengenezo, kubadilisha vifaa, ubunifu na maarifa ya kawaida. Timu maalumu kutoka Daikin italuwa ikiwatembelea wanafunzi hao ili kuhakikisha wanaielewa teknolojia hiyo vizuri.

“Kwa kupitia mpango huu, tunafundisha vizazi vijavyo vya mafundi ambao wataweza kuimudu teknolojia ya Daikin kwa weledi mkubwa na kujitengenezea nafasi kubwa ya kujiajiri au kuajiriwa,” alisema Mkuu wa Biashara wa Daikin katika ukanda wa Afrika Mashariki, Bw. Dinesh Kumar Sinha

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Don Bosco, Fr Waldemar Jonatowski aliishuru Daikin kwa kuunga mkono program hii ya mafunzo na kuongeza kuwa itaboresha maisha ya wanufaika na kuwapa maarifa mapya katika sekta inayokuwa kwa kasi.

Uhitaji wa teknolojia hii na mitambo ya HVAC inazidi kuongezeka sio Tanzania tu, bali dunia nzima kutokana na ongezeko kubwa la joto na watu wengi kukimbilia mijini. Watu wengi sasa wanafunga viyoyozi majumbani mwao hivi ni muhimu kuwa na mafundi waliobobea katika teknolojia hii ya HVAC.

“Tunaishukuru Daikin Kwa kushirikiana na sisi katika kutoa mafunzo kwa vijana wenye uhitaji ili wapate maarifa kwani hili litawafanya wawe bora zaidi katika soko la ajira. Maarifa wanayoyapata hapa yatawasaidia kutanua fursa zao na kuboresha maisha ya jamii zao,”alisema Fr Jonatowski.

Don Bosco inatoa mafunzo ya ufundi ikiwemo maadili na elimu ya kijamii kwa vijana wa kike na kiume wa kati ya umri wa miaka 18-24. Pamoja na kutoa vyeti vya mafunzo ya ufundi, chuo hicho kinalenga kutoa elimu ya maarifa ya kijamii kwa wanafunzi.

Kwa mujibu wa Bw. Sinha, kampuni yake ilichagua kushirikiana na Chuo cha Don Bosco kwa sababu ya mfumo wa ufundishaji wa chuo hicho.

“Hali ya nidhamu katika Chuo cha Don Bosco na uamuzi wao wa kumjenga mwanafunzi katika nyanja zote inawafanya wawe wabia wazuri katika kuendesha kituo kama hiki cha ufanisi (center of excellence). Licha ya kuwajengea vijana maarifa katika teknolojia hii ya HVAC, program hii pia inatoa mafunzo ya ujasiriamali na maarifa ya kijamii,” alisema Bw. Sinha

Alisema, kampuni yake inajivunia katika maisha bora endelevu katika jamii ikiwemo kuchangia suala la elimu.

“Mchango wetu katika jamii unalenga katika kuchangia katika mikakati mbalimbali ya elimu ambayo inatoa fursa mbalimbali kwa wanafunzi. Kupitia miradi yetu ya kijamii, tunachangia katika elimu kwa vizazi vya kesho ili kukuza teknolojia na jamii endelevu,” alisema

Mwaka jana Daikin ilizindua mradi kama huu nchini Kenya kwa kushirikiana na jamii ya Don Bosco ambapo wanufaika kutoka familia masikini walipata maarifa.

Daikin ni kampuni ya Kijapani ambayo bidhaa zake zinauzwa katika nchi 170 duniani.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...