Katika jitihada za kuongeza matumizi ya simu za mkononi nchini, kampuni ya teknolojia na mawasiliano, Vodacom Tanzania PLC imeshirikiana na Infinix kuzindua toleo jipya la simu aina ya Infinix HOT 30 ambayo itaambatana na kampeni maalum kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

Kuongeza matumizi ya simu janja ni moja ya chachu kwa Vodacom kufikia mafanikio ya adhma yake ya kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali, ambapo kampuni inalenga kutoa simujanja zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu. Na hii ndiyo sababu mojawapo ya kushirikiana na Infinix kuhakikisha kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu wanashiriki kikamilifu katika jamii ya kidijitali ambayo taifa linafanya jitihada kubwa kuijenga.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, George Lugata amesema, “Vodacom ina historia kubwa katika uendelezaji na uongezaji wa upatikanaji wa huduma za kiteknolojia kupitia simu. Tunaishi katika ulimwengu unaotaka kutuunganisha pamoja ambapo simu za kisasa sio anasa tena; bali ni hitaji muhimu la kiuchumi. Simujanja huwawezesha watu kuwasiliana, kujenga urafiki na pia kunufaika na fursa kadha wa kadha zinazotuzunguka ukilinganisha na kipindi cha nyuma.”

Bw. Lugata aliongeza kuwa Vodacom, inaamini kuwa kila mtu anastahili kumiliki simujanja zenye ubora na ndio sababu kampuni hiyo inakuja na vumbuzi mbalimbali ili kumuwezesha kila Mtanzania kumiliki simujanja. Aliendelea kuwa kampuni itawazawadia wateja watakaonunua simu hii 96GB kwa muda wa miezi 12 ili kufurahia huduma za kidijitali zinazotolewa na Mtandao Supa.

Kukuza udadisi na kushirikishana maarifa miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu, Vodacom kwa kushirikiana na Infinix wataendesha ‘Chemsha Bongo’ kwa vyuo vinne vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam ambavyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Bw. Lugata ameonesha kujivunia ukurasa mpya wa upatikanaji wa simu nafuu ambazo wamezindua kwa wateja na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi kupitia Mtandao Supa ambapo kwa sasa unaendesha kampeni ya ‘Zaidi ya Mtandao’ iliyojikita katika kudhihirisha utoaji wa huduma na bidhaa zenye manufaa kwa Watanzania wote nchini.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Infinix, Eric Mkomoya amesema kuwa, “Infinix ni kampuni yenye mafanikio inayojulikana kimataifa. Leo tunayo furaha kubwa kuwatangazia ujio mpya wa Infinix HOT 30 yenye maboresho ya hali ya juu kwa wapenzi wa michezo na burudani za kwenye simu ikiwa imekuja na ‘8-core Helio G88 chip’ ikiwa na ‘ARM Cortex-A75 cores’ mbili zenye nguvu kufanya kazi kwa kasi ya juu mpaka kufikia 2.0GHz. Pia ina teknolojia bunifu ya kuongeza uwezo wa kuhifadhi vitu, kutoka 8GB iliyonayo mpaka kufikia 16 GB. Matokeo yake inawezesha kuwaka kwa haraka na uwezo wa kuruhusu applikesheni zingine kufanya kazi, kuwapatia watumiaji urahisi wa kutumia kwa ufanisi bila kuathiri matumizi mengine."

Mkomoya alifafanua kuwa Infinix HOT 30 imekuja na teknolojia ya kuchaji ya 33W yenye betri yenye uwezo wa 5000mAh hivyo kufanya kikomo cha matumizi ya betri kuendelea kudumu kwa muda mrefu. Imekwishafanyiwa majaribio kuona betri ya simu itadumu kwa muda gani kupitia programu tofauti maarufu kama vile za filamu, michezo na burudani, na video fupi. Na kwa ufanisi kwenye picha angavu, simu hii ina 90Hz ambayo huboresha matumizi mara kwa mara ili mtumiaji aendelee kufurahia.

‘Chemsha Bongo’ kwa wanafunzi wa vyuo vikuu itaendeshwa kwa muda wa wiki nne ambapo washindi wataondoka na simu za Infinix HOT 30. Kwa kuongezea, wataweza kununua simu hizi mpya kwa punguzo la bei ndani ya kipindi ambacho ya zoezi hili kwenye maeneo yao ya vyuo.


Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc, Bw. George Lugata (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu ya Infinix HOT 30 kwa kushirikiana na Infinix Tanzania uliofanyika kwenye duka la Voda Shop lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki iliyopita. Wakimsikiliza kwa makini, kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Infinix Tanzania, Bw. Eric Mkomoya na kulia ni mzungumza wa lugha za alama, Bi. Fatna Salim Kaeza.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Infinix Tanzania, Bw. Eric Mkomoya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu ya Infinix HOT 30 kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania uliofanyika kwenye duka la Voda Shop lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam mwisho mwa wiki iliyopita. Katikati ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc, Bw. George Lugata, na kulia ni mzungumza wa lugha za alama, Bi. Fatna Salim Kaeza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...