Na Elias Gamaya, Shinyanga.
Wakurugenzi na wakuu wa idara za lishe Wilaya ya Shinyanga Mkoani Shinyanga wametakiwa kuzingatia suala la lishe kwa wanafunzi wa shule za msingi na Shule za sekondari wilayani humo wawapo mashuleni ili kuwajengea afya bora na kuepukana na magonjwa ya utapiamlo na Udumavu yanayozoofisha Afya za watoto
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh. Johari Samizi wakati akipokea tathmini ya lishe kwa wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari kwa maafisa lishe wote na wakuu wa Idara ya lishe wilayani shinyanga.
"Ili tuwe na taifa zuri lazima tuzingatie lishe kwa watoto wetu, tunaweza kuwachapa wanafunzi kumbe wameshadumaa kwa sababu ya kukosa chakula tujitahidi sana hawa wanafunzi wapate chakula ili tuimalishe afya za watoto wetu" amesema Mkuu huyo wa wilaya Shinyanga
Afisa lishe mkoa wa shinyanga Yusuph Hamisi amesema kwa wilaya ya Shinyanga bado hali si nzuri sana kwa upande wa utoaji wa Chakula kwa wanafunzi hii inasababishwa na wazazi kutoivisha chakula kwa mwaka huu.
"Kwa manispaa ya Shinyanga kwa takwimu za mwezi januari hadi machi 2023 zinaonyesha bado asilimia 40% utoaji wa chakula hii inasababishwa na kutoivisha vyakula kwa wazazi " amesema Yusuph Hamisi Afisa lishe Mkoa wa Shinyanga.
Michuzi blog imezungumza na baadhi ya wanafunzi shule za sekondari na shule za msingi manispaa ya shinyanga zinazotekeleza utoaji wa chakula kwa wanafunzi ambapo wameeleza namna ambavyo walikua wanapata adha ikiwemo kutofanya vizuri kwa wanafunzi kutokana na kushinda njaa, kuingiwa kwa vishawishi vya ngono ili kupata hela ya kununua chakula pindi wanapukua shuleni
"Tulikua tunakaa njaa hadi saa nane ambapo mwalimu akiwa anafundisha mchana wanafunzi wengine wanasinzia darasani hatumielewi, hali ambayo ilikua inawafanya kwa baadhi ya wanafunzi kujiingiza kwenye mahusiano ili kupewa hela ya chakula na watu wao pindi wanapokua Shuleni. Wamesena wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh. Johari Samizi (juu) akiongea na Maafisa Lishe wilayani humo
Maafisa Lishe wakiwa kwenye kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh. Johari Samizi (juu) akiendelea kutoa maelekezo
Afisa lishe mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamisi akitoa maelezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...