Na. Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2023/24 umetoa maelekezo kwa Maafisa Masuuli kuzingatia masuala ya Jinsia, wakati wa uandaaji, uwasilishaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini pamoja na utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Mpango na Bajeti zao.

Haya yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mhe. Halima James Mdee aliyetaka kujua muda ambao Serikali itaanza kutengeneza bajeti kwa jicho la jinsia.

Mhe. Chande alisema pamoja na maelekezo hayo, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake - UN Women, inaendelea kushirikiana na Serikali kujenga uwezo katika maandalizi ya nyaraka za sera kwa kuzingatia masuala ya kijinsia.

Alisema katika mwaka 2022/23, Wizara ya Fedha na Mipango imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kuboresha Mwongozo wa maandalizi ya mipango na bajeti ya Serikali kwa jicho la kijinsia.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali Bungeni, jijini Dodoma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...