Na Elias Gamaya wa Michuzi TV, Shinyanga
3/5/2023.
Mgodi wa williamson Diamond limited( WDL)uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umeagizwa kukamilisha ujenzi wa mabwawa ambayo yanaweza kudumu kwa muda mrefu ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha hasara na kupelekea serikali kukosa mapato.
akitoa maagizo hayo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Chiristina Mdeme alipotembelea mgodi huo kuona hatua zilizochukuliwa tangu bwawa la maji tope lilipopasuka Novemba saba 2022 na kusababisha athari kwa wakazi wa maeneo hayo.
''Tumeathiri hata ajira za watu wengine ambao walikuwa wanatoa huduma kwenye mgodi, ni vyema sasa mkahakikisha bwawa hili linajengwa kwa kiwango ili isitokee tena kupasuka'' amesema mkuu wa mkoa wa shinyanga Bi Chiristna Mdeme.
Kwa upande wake Mhandisi mkuu wa mgodi wa williamson Diamond limited (WDL) Mipawa Shagembe amesema ulianza Machi mwaka huu na unatarajia kukamilika mwezi julai mwaka huu ili kuanza shughuli za uzalishaji mwezi agosti mwaka 2023.
Meneja mkuu wa wa mgodi huo Ayoub Mwenda amesema tayari wamejenga kingo kwenye bwawa hilo ili kuzuia tope kutoka nje huku meneja ulinzi mgodi Zefania Mwashitete akaeleza changamoto za wananchi kuvamia mgodi huo.

Bwawa linalojengwa
Kazi zikiendelea mgodini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...