NA FARIDA MANGUBE, MICHUZI TV
Watu wanne wa familia moja Kijiji cha Malola B Kata ya Malola Tarafa ya Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wamefariki baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuungua Moto usiku wa kuamkia Mai 5, 2023.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amefika eneo la tukio na kuthibisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema bado uchunguzi unaendele ili kubaini chanzo cha tukio Hilo.
Aidha Kamanda amewataja waliofariki ni Amani Malekela (72) ambaye ni Baba wa familia hiyo, Habiba Aman ( 10), Sadick Amna (8) na Bahati Aman( 5).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...