Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV- Chamwino

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa miezi miwili na nusu mradi wa maji Handali uliopo katika Jimbo la Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma uwe umekamilika ili wananchi wapate maji.

Chongolo ametoa maagizo hayo leo Juni 18,2023 alipotembelea mradi huo na kuelekezwa kwamba umeshindwa kukamilika na hivyo kusababisha changamoto ya uhaba wa maji kwa wananchi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa Katibu Mkuu Chongolo imeeleza kuwa mradi huo hadi utakapokamilika unatarajia kugharimu zaidi ya Sh.milioni 600 na utawezesha watu 8000 kupata maji safi na salama

Baada ya kutolewa kwa taarifa kuhusu mradi huo ndipo Chongolo pamoja na maelekezo mengine ametoa miezi miwili na nusu uwe umekamilika na wananchi waanze kupata maji."Mradi huu ndani ya miezi miwili na nusu uwe umekamilika, sio kila siku kuoneshwa michoro ya ramani ya ujenzi."

Akielezea zaidi Chongolo amewaagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma kuhakikisha maagizo yake yanatekelezwa.

Chongolo ambaye yupo wilayani Chamwino ameendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020-2025 pamoja na kukagua uhai wa Chama na kutatua changamoto za wananchi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...