Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo amewataka
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kutambua na kutimiza
wajibu mkubwa walionao kwa chama hicho, hasa katika kukilinda na
kukisemea ili kizidi kuwa imara na kizidi kuaminiwa kubeba dhamana ya
kutawala na kuongoza nchi.
Ndugu Chongolo amesisitiza pia kuwa
Chama Cha Mapinduzi kinawategemea vijana hao wa UVCCM kutumia nafasi
zao, kubeba agenda za Chama zenye maslahi kwa taifa na Watanzania, na
kamwe wasikubali kuhusishwa kuwa sehemu ya kubeba maslahi binafsi ya
watu wachache, wenye ndoto zinazokinzana na misingi ya Chama.
Katibu
Mkuu Chongolo ameyasema hayo leo Jumanne, Juni 27, 2023, alipokuwa
akihutubia Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM, waliokutana
katika kikao chao cha kawaida, kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Chama
Cha Mapinduzi (NEC) Taifa, jijini Dodoma.
“Chama chetu…Chama Cha
Mapinduzi kinawategemea sana Jumuiya ya Umoja wa Vijana Tanzania.
Kinawategemea kukilinda na kukisemea na kufanya mambo yakayokifanya
kiendelee kuwa chama tawala nchini na si vinginevyo. Tusiache wajibu
huo. Tusiache kulinda viongozi wetu. Tusibebe jukumu la kuwa viongozi wa
watu. Narudia kwa kusisitiza. Tuwe viongozi wa jumuiya."
“Hasara
ya kuwa kiongozi wa mtu…ni hasara unayojitengenezea kuwa daraja la
kukuharibia kesho yako. Ukiwa kiongozi unayesimama na kujitegemea,
utaishi miaka yote ukiwa unaendelea kufaidi fursa ya uongozi
uliojitengenezea mwenyewe. Lakini ukiamua kuwa kiongozi mfuasi wa mtu,
yule mtu akiondoka, na wewe unakwenda na maji. Na mara nyingi watu
tunaowafuasia ni watu wenye ndoto,” amesema Ndugu Chongolo na kuongeza;
“Kuna
watu maisha yao ni ndoto na ni ndoto kweli kweli. Acheni na achaneni na
ndoto za watu. Ishini na ndoto za uhakika, ndoto za taasisi…ndoto za
CCM. Simameni na viongozi halali na sahihi wa taasisi na sio viongozi
wanaojiandaa kuwa viongozi bila kuandaliwa na taasisi. Viongozi wengi
wanaojiandaa na kuwa na tamaa ya nafasi, kwenye chama hiki huwa hawapati
nafasi. Nendeni kwenye historia. Sasa ninyi msiwe wafuasi wa
wanaojiandaa. Kuweni wafuasi wa taasisi.”
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Mohamed Ali Mohamed Kawaida, ametoa
wito kwa wajumbe wa kikao hicho, ambao ni pamoja na Wenyeviti wa UVCCM
Mikoa, Makatibu wa UVCCM Mikoa na Wajumbe wa Baraza kutoka mikoa yote ya
Kichama, Tanzania Bara na Zanzibar, kuhakikisha wanaketi na kusimamia
vikao vya ngazi zao hadi chini na kufanya ziara za kuimarisha jumuiya
hiyo katika ngazi zote.
“Nitoe wito na kwenu na ninyi mnavyo
vikao vyenu kule chini, kwa Wenyeviti, Makatibu pamoja na Wajumbe wa
Baraza Kuu. Niwaombeni sana mkasimamie vikao hivyo, viendelee na
vifanyike. Kwa sababu kwenye vikao ndipo tunapotoka na maazimio sote ya
pamoja, kauli ya pamoja na uelewa wa pamoja.”
“Lakini sambamba na
hilo, niwekee mkazo katika suala zima la ziara. Niwapongeze baadhi ya
maeneo, nimekuwa nikiwafuatilieni kwa karibu. Mmekuwa mkifanya ziara
katika maeneo yenu. Niwaombe kwa wale bado. Ziara hizo zikaanze au
zikaendelee. Na zira hizo zikianza ama zikiendelea, basi zisiwe ziara za
kupiga picha bali ziwe ziara za kuleta tija katika chama chetu na kwa
Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi,” amesema Ndugu KawaidaKatibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akihutubia
Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
katika kikao cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kuu
ya CCM Taifa (White House), CCM Makao Makuu Dodoma.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo
na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM)
Ndugu Mohamed Ali Mohamed maarufu Kawaida (kushoto) wakati wa Kikao cha
Kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kawaida
kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (White
House), CCM Makao Makuu Dodoma.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM)
Ndugu Mohamed Ali Mohamed maarufu Kawaida akizungumza wakati wa
kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu
Daniel Chongolo
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi waliohudhuria kikao hicho katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa (White House), CCM Makao Makuu Dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...